Majeshi ya Somalia na yale ya Umoja wa
Afrika (AU) wamekomboa miji kadhaa kutoka kwa wanamgambo wa Al-shabab
katika kile walichokiita juhudi mpya za kuliondoa kundi hilo kutoka
kwenye ngome zake nchini humo.
Moja ya maeneo ni katika mji wa
Burdhubo ambao ulikuwa ni ngome kuu ya Alshabab kusini mwa Somalia.
Majeshi kutoka Umoja wa Afrika nchini Somalia yajulikanayo kama AMISOM
na jeshi la taifa la Somalia yalichukua tena udhibiti wa eneo hilo
Jumapili baada ya siku moja ya mapigano.
Kanali Ali Hamud msemaji wa AMISOM
aliimbia VOA kwamba wapiganaji wa Alshabab wanarudi nyuma mara tu
wanapoona majeshi ya AMISOM, lakini hilo bado linaangaliwa ikiwa badala
yake wanajipanga kwa vita vya msituni.
Miji mingine ambayo jeshi la Somalia
na AMISOM wamekomboa tangu Ijumaa ni pamoja na Weel Dehyn,Wajid,Rabdhure
Ted na Hudur. Wako katika mikoa ya Gedo na Bakool karibu na mpaka wa
Ethiopia na kilometa chache kutoka mji mkuu wa Somalia Mogadishu.
Chanzo: VOA
0 comments:
Post a Comment