Mwili wa mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Ipembe mjini Singida Rashid
Said (16) (kushoto) na wa kijana ambaye hajafahamika jina aliyekuwa
anajaribu kumwokoa mwanafunzi.Vijana hao wawili waliofariki dunia Machi
08 mwaka huu saa nane mchana ,mwanafunzi huyo amefariki dunia baada ya
Mtumbwi waliokuwa wameupanda kupigwa na upepo na wao kutumbukia ndani ya
maji.
Mwili
wa mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya sekondari Ipembe Rashid
Said, ukiingizwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya
mkoa mjini Singida.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
MWANAFUNZI
wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Ipembe mjini
hapa,Rashid Saidi (16) amefariki dunia baada ya mtumbwi aliokuwa
umeupanda ziwani, yeye na baadhi ya wanafunzi wenzake kupigwa na upepo
mkali na kusababisha mtumbwi kupinduka na wao kutumbukia kwenye maji.
Kijana
mmoja ambaye sio mwanafunzi na jina lake bado halijapatikana,alijitolea
kumwokoa mwanafunzi huyo,lakini naye kwa bahati mbaya alifariki dunia
baada ya kunywa maji mengi na kuzama ziwani.Tukio hilo la kusikitisha
limetokea machi nane mwaka huu saa nane mchana.
Inadaiwa kuwa wanafunzi hao baada ya kumaliza kipindi cha’tuition’ shuleni kwao,kama kawaida yao walienda ‘pikiniki’ katika ziwa la Kindai na kuanza kuogelea pembeni mwa ziwa hilo.
Askari kutoka kikosi cha zima moto
mjini hapa,Bahati Hemed,amesema kwa mujibu wa taarifa alizopewa na
mashuhuda wa tukio hilo,ni kwamba baada ya wanafunzi hao kumwagwa ndani
ya maji,baadhi ya wanafunzi walifanikiwa kujiokoa na Rashid ambaye hana
uzoefu wa kuogelea,alizama nada ya maji.
Amesema
wanafunzi hao baada ya kutoka nje ya ziwa,walimwomba kijana mmoja
ambaye alikuwa na umri mkubwa aingie ziwani ili akamwokoe mwanzao.
“Yule
kijana aliyejitolea kumwokoa mwanafunzi,alipokaribia alikotumbukia
mwanafunzi huyo,na yeye mambo yalimwendea vibaya na hivyo kutupikia
ndani ya maji na kusababaisha na yeye apoteze maisha yake”alisema Bahati
kwa masikitiko.
Alisema
baada ya hapo waliweza kuita wavuvi ambao walifika na nyavu na kuwaza
kutoa miili hiyo miwili kutoka ndani ya ziwa Kindai.
0 comments:
Post a Comment