MABINGWA wa Ulaya, Bayern Munich
wanaweza kuadhibiwa na UEFA baada ya kikundi cha mashabiki wake
kupeperusha bango la udhalilishaji kwa wapinzani wao, Arsenal wakati wa
mchezo wa marudiano Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya jana Uwanja
wa Allianza Arena, tkimu hizo zikitoka sare ya 1-1.
Kwa
matokeo hayo,Bayern wamesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1
baada ya awali kushinda 2-0 Uwanja wa Emirates mjini London.
Bango
hilo lilikuwa linasomeka 'Gay Gunners' yaani Mashoga Gunners na
lilionekana kumlenga kiungo Mesut Ozil likipeperushwa kabla ya mechi
kuanza Uwanja wa Allianz Arena.
Licha
ya kuwa na namba ya kudumu kwenye kikosi cha kocha Joachim Low wa timu
ya taifa ya Ujerumani, kiwango cha uchezaji cha Ozil siku za karibuni
katika kikosi cha Arsene Wenger
kinatiliwa shaka na mashabiki wake nchini mwake na vyombo vya habari
vinautazama kwa jicho la tatu uwezekano wa kupata nafasi katika kikosi
kitakachokwenda Brazil kwenye Kombe la Dunia.
0 comments:
Post a Comment