>JUMAPILI: MAN UNITED v LIVERPOOL, SPURS v ARSENAL!
>>JUMAMOSI: VINARA CHELSEA VILLA PARK NA VILLA!!
WIKIENDI ZIPO Mechi 10 za Ligi Kuu
England, Timu zote 20 dimbani, lakini ‘Habari ya Mujini’ ni SUPA SANDE
wakati BIGI MECHI mbili, Manchester United v Liverpool, na ile Dabi ya
London ya Kaskazini, Tottenham v Arsenal, zitakapokuwa Mechi pekee.
PATA TAARIFA/DONDOO/RATIBA:
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Machi 15
1545 Hull v Man City
1800 Everton v Cardiff
1800 Fulham v Newcastle
1800 Southampton v Norwich
1800 Stoke v West Ham
1800 Sunderland v Crystal Palace
1800 Swansea v West Brom
2030 Aston Villa v Chelsea
Jumapili Machi 16
1630 Man United v Liverpool
1900 Tottenham v Arsenal
SUPA SANDE-Jumapili Machi 16
MANCHESTER UNITED v LIVERPOOL
-Old Trafford
IMEZOELEKA, kwenye Ligi Kuu England, kila Mechi hii ikifika, ni Man United ndio wanawania Ubingwa
na Liverpool ndio wasindikizaji lakini safari hii, licha ya Man United
kuwa ndio Mabingwa Watetezi, Liverpool ndio wanaowania Ubingwa na Man
United sasa wanapigania walau waingie 4 Bora.
Hii ni Mechi ya 42 kwa Man United Msimu
huu na pengine hii itakuwa mara ya 42 kwa Meneja wao David Moyes kutaja
Kikosi tofauti kwa mara nyingine tena tofauti na Liverpool ambao panga
pangua wamo Luis Suarez, Daniel Sturridge na Raheem Sterling.
TAKWIMU MUHIMU=
MAN UNITED v LIVERPOOL
VIKOMBE-Jumla:
LIVERPOOL 59 [Ubingwa England=18]
MAN UNITED 62 [Ubingwa England=20]
MECHI-Uso kwa Uso
LIVERPOOL=Ushindi 63
MAN UNITED=Ushindi 75
SARE=51
MECHI 6 ZILIZOPITA:
11 FEB 2012 Man United 2 Liverpool 1
23 Sep 2012 Liverpool 1 Man United 2
13 Jan 2013 Man United 2 Liverpool 1
1 Sep 2013 Liverpool 1 Man United 0
25 Sep 2013 Man United 1 Liverpool 0
Huku Jumatano wakikabiliwa na Mechi
muhimu ya UEFA CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Olympiakos ambao walishinda 2-0,
ni vigumu kujua Moyes atapanga Kikosi kipi hasa kwa vile atataka
kupindua kipigo cha Bao hizo 2-0 Siku ya Jumatano.
Hata hivyo, kama alivyonena Mchezaji wa
zamani wa Man United, Gary Neville, ambae sasa ni Mchambuzi wa Sky
Sports, kwamba: “Sikubali Gemu na Olympiakos ndio yenye presha kubwa.
Nadhani hata Mashabiki wa Man United hapo Jijini kwao hawadhani kama
watafuzu UCL. Kitu ambacho Mashabiki hao hawataki ni fedheha Jumamosi au
Jumanne. Hawataki Wapinzani wao wa Jadi watue Old Trafford na
kuwaonyesha wao ni wabovu kama walivyokuwa kwenye baadhi ya Mechi Msimu
huu.”
Itakuwa kujitia kitanzi shingoni kwa Moyes kuboronga katika upangaji Kikosi.
TOTTENHAM v ARSENAL
-White Hart Lane
Tottenham na Arsenal zote zinatoka
kwenye Mechi za Ulaya zote zikiwa na vipigo na kwa Arsenal ni kubwagwa
nje ya UEFA CHAMPIONZ LIGI baada kufungwa Jumla ya Mabao 3-1 na Mabingwa
Watetezi, Bayern Munich, wakati Tottenham wamechapwa 3-1 na Benfica kwenye Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya EUROPA LIGI.
Wiki iliyopita, kwenye Ligi, Tottenham walichapwa 4-0 na Chelsea kwenye Ligi na kuibomoa azma yao ya kumaliza 4 Bora.
Hii ni Mechi muhimu kwa Arsenal kushinda kwani Mwezi huu wanakabiliwa na Mechi nyingine nzito dhidi ya Chelsea na Man City.
Jumamosi Machi 15
HULL CITY v MAN CITY
-KC Stadium
Ndoto ya kutwaa Mataji manne kwa Man
City Msimu huu imeyeyuka baada, ndani ya Wiki moja, Wiki hii, kubwagwa
nje ya FA CUP na Wigan na kutupwa nje ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na
Barcelona, na sasa wamebakia na Kombe moja, CAPITAL ONE CUP, ambalo
wamelitwaa Majuzi na bado ipo ndoto ya kuwa Bingwa.
Wapo Pointi 9 nyuma ya Vinara Chelsea
ingawa wao wana Mechi 3 mkononi, hivyo Mechi hii na Hull City kwao ni
‘piga ua’ ushindi lazima.
EVERTON v CARDIFF CITY
-Goodison Park
Everton bado wana ndoto za kumaliza ndani ya 4 Bora na Cardiff City wao wanapigania uhai wao kubaki Ligi Kuu England.
Baada kubwagwa nje ya FA CUP na Arsenal
kwa kutandikwa 4-1 na Arsenal, Everton watataka kumaliza machungu yao
dhidi ya Kikosi cha Nguli wa Man United, Ole Gunnar Solskjaer, ambao
Wikiendi iliyopita waliambua ushindi wao wa pili katika Mechi 9
walipoichapa Fulham 3-1.
FULHAM v NEWCASTLE
-Craven Cottage
Fulham wako mkiani na bila ushindi
watazidi kujichimbia shimo lao na safari hii wanapambana na Newcastle
ambayo haina Meneja baada Alan Pardew kufungiwa Mechi 7 na hii ni Mechi
yake ya kwanza Kifungoni ambayo pia haruhusiwi kabisa kuwepo Uwanjani.
SOUTHAMPTON v NORWICH
-St Mary’s
Southampton hawajashinda katika Mechi
zao 3 zilizopita za Ligi Uwanjani kwao lakini wanatinga kwenye Mechi hii
wakitoka kwenye ushindi wa Ugenini walipoichapa Crstal Palace Bao 1-0.
Wikiendi iliyopita, Norwich, ambao nao si salama kwenye Ligi, walitoka Sare 1-1 na Stoke City.
STOKE v WEST HAM
-The Britannia
West Ham na Stoke, pamoja na Aston Villa, zote zina Pointi 31.
Stoke watawakosa Jonathan Walters na
Charlie Adam, wote wakiwa Kifungoni, na wanapambana na West Ham ambayo
ilishinda Mechi 4 mfululizo kabla kufungwa na Everton.
SUNDERLAND v CRYSTAL PALACE
-Stadium of Light
Hii ni Mechi muhimu kwa Timu zote mbili katika vita yao kujinusuru kushushwa Daraja.
SWANSEA v WEST BROM
-Liberty Stadium
Swansea hawajashinda katika Mechi 3 za
Ligi na wapo Pointi 4 juu ya zile Timu 3 za mkiani, pamoja na West Brom,
ambao wako Nafasi ya 4 toka mkiani, hivyo ushindi kwao ni kufa na
kupona.
West Brom, chini ya Meneja mpya, Pepe
Mel, hawajashinda hata Mechi moja na hii ni moja ya mlolongo wa Mechi
ambazo ushindi kwao unawezekana na, baada ya hii, zitafuata Mechi dhidi
ya Cardiff na Norwich, wote wakipigania uhai wao.
ASTON VILLA v CHELSEA
-Villa Park
Ushindi kwa Chelsea utawabakisha Pointi 7
au zaidi kileleni na bado Jose Mourinho, Meneja wa Chelsea, anadai wao
sio Mabingwa watarajiwa.
Baada kufungwa Mechi 4 mfululizo, Aston Villa waliibuka kwa kuitandika Norwich 4-1 katika Mechi yao ya mwisho.
MSIMAMO:
NA |
TIMU |
P |
GD |
PTS |
1 |
Chelsea |
29 |
34 |
66 |
2 |
Liverpool |
28 |
38 |
59 |
3 |
Arsenal |
28 |
24 |
59 |
4 |
Man City |
26 |
42 |
57 |
5 |
Tottenham |
29 |
0 |
53 |
6 |
Man United |
28 |
12 |
48 |
7 |
Everton |
27 |
11 |
48 |
8 |
Newcastle |
28 |
-2 |
43 |
9 |
Southampton |
30 |
2 |
42 |
10 |
West Ham |
28 |
-4 |
31 |
11 |
Aston Villa |
28 |
-7 |
31 |
12 |
Stoke |
29 |
-14 |
31 |
13 |
Hull |
28 |
-5 |
30 |
14 |
Swansea |
28 |
-4 |
29 |
15 |
Norwich |
29 |
-22 |
29 |
16 |
Crystal Palace |
28 |
-19 |
27 |
17 |
West Brom |
28 |
-11 |
25 |
19 |
Cardiff |
29 |
-28 |
25 |
18 |
Sunderland |
26 |
-16 |
24 |
20 |
Fulham |
29 |
-36 |
21 |
0 comments:
Post a Comment