Sunday, 16 March 2014

UCL: JUMANNE & JUMATANO, NANI KUSONGA ROBO FAINALI??

>>CHELSEA, MAN UNITED ZITAFUZU??

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Raundi ya Mtoano ya Timu 16
MARUDIANO
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
[Saa za Bongo]
Jumanne Machi 18
22:45 Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü [1-1]
22:45 Real Madrid CF v Schalke 04 [1-6]
Jumatano Machi 19
22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg [4-2]
22:45 Manchester United v Olympiacos CFP [0-2]

UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, Jumanne na Jumatano Usiku, itakamilisha Mechi zake 4 zilizobaki za RaundiUEFA_CHAMPS_LIGI-A_TO_DyaMtoano ya Timu 16 ili kupata Timu 4 zilizobaki kuingia Robo Fainali kuungana na Bayern Munich, Atletico Madrid, Barcelona na Paris Saint-Germain zilizofuzu Wiki iliyopita.

UEFA CHAMPIONZ LIGI
TIMU ZILIZOTINGA ROBO FAINALI:
[Bado 4]
-Bayern Munich
-Atletico Madrid
-Barcelona
-Paris Saint-Germain
Wakati Borussia Dortmund na Real Madrid zina kazi nyepesi kidogo kufuzu baada ya kushinda Mechi zao za kwanza, kibarua kikubwa kipo kwa Schalke, Zenit St. Petersburg na Manchester United kupindua vipigo huku Chelsea, wakiwa kwao Stamford Bridge, wanasaka Sare ya 0-0 au ushindi ili kuibwaga Galatasaray waliyotoka nayo Sare ya 1-1 katika Mechi ya Kwanza.
Zenit St. Petersburg walifungwa kwao 4-2 na Borrussia Dortmund na wana kibarua kigumu kushinda huko Signal Iduna Park.
Kwa Schalke, ambao walikung’utwa 6-1 na Real Madrid huko Germany, pengine kushinda Uwanjani Santiago Bernabeu ni miujiza.
Nao Mabingwa wa England, Manchester United, wana kazi nzito kupindua kipigo cha 2-0 walichopewa na Olympiakos katika Mechi ya Kwanza wakati watakaporudiana Old Trafford Jumatano Usiku.
Droo ya kupanga Mechi za Robo Fainali itafanyika huko Nyon, Uswisi hapo Ijumaa Mchana ya Machi 21.
MARUDIANO
MATOKEO:
[Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili]
Jumanne Machi 11
Bayern Munich 1 Arsenal 1 [3-1]
Atletico de Madrid 4 AC Milan 1 [5-2]
Jumatano Machi 12
FC Barcelona 2 Manchester City 1 [4-1]
Paris Saint-Germain 2 Bayer 04 Leverkusen 1 [6-1]

0 comments: