Kuanzishwa
kwa juhudi mpya za utafutaji wa ndege katika Bahari ya Hindi huenda
kukatoa sura mpya ya matumaini hasa kutokana na ripoti kuwa huenda ndege
hiyo ilibadilisha mwelekeo wa safari.
Napoli.
Mshambuliaji wa timu
ya taifa ya Italia Mario Balloteli ameelezea kukerwa na kitendo cha
Afisa Mkuu wa Mamlaka za usafiri wa Anga ya Malaysia Azharuddin Abdul
Rahman kumfananisha na abiria wawili wanaodaiwa kutumia hati bandia za
kusafiria kwenye ndege iliyopotea ya Malaysia.
Hivi karibuni wakati akitoa
taarifa kwa waandishi wa habari kuhusiana na watu wanaodaiwa kutumia
hati bandia kwenye ndege iliyopotea, Rahman alisema kuwa watu hao
walikuwa wamefanana kwa sura na mchezaji huyo wa AC Milan.
Ofisa huyo alifafanua kuwa
“abiria waliotumia hati bandia za kusafiria na kisha kuingia kwenye
ndege hiyo aina ya MH370 ya Shirika la Ndege Malaysia wanafanana na
Balotelli.”
Balotteli anadaiwa kusema ni
jambo la kuudhi kuona Bw Rahma akimfananisha na wahalifu licha ya
kutokuwa na abiria mweusi katika ndege hiyo.
Balloteli ambaye ni mmoja ya
wachezaji wanaotajwa kuwa na vituko zaidi uwanjani amemtaka ofisa huyo
kuomba radhi haraka iwezekanavyo.
Msako wa ndege sasa wahamia Bahari ya Hindi
Kusoma zaidi bofya hapa chini
0 comments:
Post a Comment