“PRESS RELEASE” TAREHE 15.03.2014.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAKAMATA PIKIPIKI MOJA MALI YA
WIZI NA VIFAA MBALIMBALI VYA KOMPYUTA.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA TAREHE 14.03.2014
MAJIRA YA SAA 04:00 USIKU HUKO KATIKA ENEO LA VWAWA, KATA NA TARAFA YA
VWAWA, WILAYA YA MBOZI LAKAMATA PIKIPIKI MOJA YENYE NAMBA ZA USAJILI
T.575 CET AINA YA T-BETTER, CPU KUMI [10] ZA KOMPYUTA PAMOJA NA KEY BOARD
MOJA MALI ZA WIZI. KATI YA MALI HIZO CPU ZIMETAMBULIWA. MTUHUMIWA
ALIKIMBIA MARA BAADA YA KUONA ASKARI, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
AIDHA
KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA TAREHE 14.03.2014 MAJIRA YA SAA 06:30 ALFAJIRI
KATIKA ENEO LA IYELA-AIRPORT, KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA JIJI NA
MKOA WA MBEYA, MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FRANSIS JOHN (21)
MKAZI WA IYELA ALIKAMATWA AKIWA NA BHANGI KETE 04 SAWA NA UZITO WA GRAM
20. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI WA BHANGI HIYO, TARATIBU ZA KISHERIA
ZINAFANYIKA IKIWA NI PAMOJA NA KUMFIKSHA MAHAKAMANI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA KWA JESHI LA POLISI ILI
MTUHUMIWA WA TUKIO LA WIZI AWEZE KUKAMATWA. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMIII
KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI
KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment