Kwa mujibu wa orodha iliyotumwa na
CAF kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Watanzania hao ni Alfred
Kishongole Rwiza wa Mwanza na Hafidh Ali Tahir wa Zanzibar ambao wamerejeshwa
tena kwenye jopo hilo.
Rwiza na Tahir ambao ni waamuzi
wastaafu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na wakufunzi wa
uamuzi walikuwepo kwenye jopo lililopita la 2012 hadi 2014.
Makamishna wapya kwa upande wa
wanawake ni Elizabeth Mwanguku Kalinga wa Mbeya na Isabellah Hussein Kapera wa
Dar es Salaam. Kamishna mwingine mpya kwa upande wa wanaume ni Muhsin Ali Rajab
kutoka Zanzibar.
Wakati huo huo, CAF imeandaa semina
kwa makamishna wanaume itakayofanyika jijini Cairo, Misri kuanzia Aprili 3 hadi
4 mwaka huu.
Watoa mada kwenye semina hiyo ya siku
mbili ni Katibu Mkuu wa CAF, Hicham El Amrani, Mkurugenzi wa Mashindano wa CAF,
Shereen Arafa na Naibu Mkurugenzi wa Mashindano wa CAF, Khaled Nassar.
Wengine ni Meneja wa Waamuzi wa CAF, Eddy Maillet, Mkurugenzi wa Habari wa CAF, Junior Binyam, Mkurugenzi wa Teknolojia ya Mawasiliano wa CAF, Tarek el Deeb na Mkurugenzi wa Masoko na Televisheni wa CAF, Amr Shaheen.
0 comments:
Post a Comment