>>’NATEGEMEA TUTAPATA NAFASI YA KUCHEZA 11 DHIDI YA 11!’
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
MARUDIANO
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
Jumanne Machi 11
[Saa za Bongo]
22:45 Bayern Munich v Arsenal FC [2-0]
22:45 Atletico de Madrid v AC Milan [1-0]
Akiongea
kabla ya Mechi yao ya Marudiano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI,UCL, ya Usiku
huu huko Allianz Arena, Munich dhidi ya Mabingwa wa Ulaya Bayern Munich,
Arsène Wenger ametaka kuwepo na haki kutoka kwa Refa.
Refa wa Mechi hii ya Leo kati ya Arsenal na Bayern ni Svein Oddvar Moen, mwenye Miaka 35, na anaetoka Norway.
Wenger alikumbushia walivyokuwa wakionewa na Marefa kwenye Mechi zao za nyuma za UCL.
Meneja huyo awa Arsenal alikumbushia
jinsi Kipa wake Wojciech Szczesny apolitolewa nje kwa Kadi Nyekundu
walipofungwa 2-0 huko Emirates katika Mechi ya kwanza na Bayern Wiki 3
zilizopita na pia kuyataja matukio ya nyuma kwenye UCL ambapo Mwaka 2006
kwenye Fainali na Barcelona Kipa wao Jens Lehmann
alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu na pia Mwaka 2011 huko Nou Camp na
Barcelona jinsi Robin van Persie alivyopewa Kadi ya Njano ya Pili kwa
kucheza Mpira baada Filimbi kulia na kutolewa kwa Kadi Nyekundu.
Wenger amesema: “Tumecheza mara kadhaa
Ulaya tukiwa Mtu 10! Safari hii natumaini haki itatendeka na tutacheza
11 dhidi ya 11 mpaka mwisho!”
Kwenye Mechi ya Leo, Wenger amesema
Kieran Gibbs atakuwa nje akiwa na maumivu ya Enka na atalazimika
kumchezesha Thomas Vermaelen kwenye Nafasi ya Fulbeki wa Kushoto kwa
vile Nacho Monreal nae pia ni Majeruhi.
Hata hivyo, Wenger ametamka kuwa wanao
uwezo wa kuwafunga Bayern Munich kwao Allianz Arena baada ya kufanya
hivyo Msimu uliopita kwenye hatua kama hii ya UCL walipofungwa 3-1
Emirates na kuichapa Bayern 2-0 katika Marudiano na kutolewa kwa Magoli
ya Ugenini.
Amesema: “Tumeshawahi kushinda hapa
kabla hivyo tunajua tunaweza kufanya tena. Ingawa Takwimu zinatupinga
lakini tulifanya Mwaka 2003 tulipoishinda Inter Milan 5-1 San Siro!”
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
MARUDIANO
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
[Saa za Bongo]
Jumatano Machi 12
22:45 FC Barcelona v Manchester City [2-0]
22:45 Paris Saint-Germain v Bayer 04 Leverkusen [4-0]
Jumanne Machi 18
22:45 Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü [1-1]
22:45 Real Madrid CF v Schalke 04 [1-6]
Jumatano Machi 19
22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg [4-2]
22:45 Manchester United v Olympiacos CFP [0-2]
0 comments:
Post a Comment