SOMA ZAIDI:
Release No. 041
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Machi 10, 2014
WANAOFANYA VUFO, UHARIBIFU VIWANJANI KUKIONA
Tunaiomba radhi Serikali kwa uharibifu 
wa viti uliotokea kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga 
ya Tanzania na Al Ahly ya Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es 
Salaam.
Uharibifu huo wa viti umesababisha 
hasara ya sh. milioni 15 kwa wamiliki wa uwanja huo ambao ni Serikali. 
TFF tutalipa fedha hizo kwa Serikali kutokana na uharibifu huo.
Tunaendelea kuchunguza tukio hilo, huku 
tukijiandaa kutoa adhabu kwa klabu na washabiki husika kulingana na 
kanuni zetu. Adhabu itakuwa kali ili iwe fundisho kwa wengine.
Kwa mujibu wa Serikali, viti kumi 
viling’olewa na kutupwa ovyo ovyo uwanjani wakati vingine 40 
viliathirika kutokana na vurugu za watazamaji hao.
Tumebeba dhamana ya kulipa uharibifu huo
 kwa vile TFF ndiyo wenye dhamana ya kusimamia mechi za kimataifa, na 
ndiyo tulioomba idhidi ya kutumia uwanja huo.
Kwa vile sasa baadhi ya washabiki, 
wapenzi na wanachama wa klabu mbalimbali nchini wanataka kufanya suala 
la uharibifu kuwa la kawaida na mazoea, Serikali inakusudia kuchukua 
mapato yote ya mchezo husika endapo kutatokea uharibifu.
Pia kuruhusu uwanja kutumiwa bila 
watazamaji kwa baadhi ya mechi, na kutoruhusu uwanja huo kutotumika 
kabisa kwa baadhi ya mechi.
Boniface Wambura Mgoyo
Media and Communications Officer
Tanzania Football Federation (TFF)
 






 
 
 
 






0 comments:
Post a Comment