Fatou Bensouda
Mwendesha
mashtaka mkuu wa mahakama ya Kimataifa ya uhalifu ICC, Fatou Bensouda
amesema huenda akakata rufaa hukumu iliyotolewa kwa mbabe wa zamani wa
kivita nchini Congo Germain Katanga.
Katanga
alipatikana na hatia nne za uhalifu wa kivita na hatia moja ya uhalifu
dhidi ya binadamu, lakini akaondolea makosa kuhusu ubakaji.
Wapiganaji wake walishutumiwa kuwabaka wanawake na kuwateka huku wakiwatumia kama watumwa wa ngono.
Makundi
ya wanawake nchini Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo yameelezea hasira na
masikitiko yao kutokana na hatua ya mahakama hiyo ya ICC ya kumuondolea
Bwana Gatanga makosa hayo.
Wakati wa
ziara yake katika mji mkuu wa DRC, Kinshasa, Bensouda alisema kuwa
huenda akakata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama.
''Majaji
hawakumuhumu kuhusiana na mashtaka ya unyanyazaji wa kimapenzi, mashtaka
ambayo tulikuwa tumemshtaki nayo, pamoja na ile ya kuwasajili watoto
jeshini'' Alisema Bensouda.
Bensouda,
amesema kuwa wanachunguza hukumu hiyo kwa undani na kuchunguza ikiwa
kuna dosari kadhaa za kisheria ambazo wanaweza kutumia kukata rufaa.
''Majaji
kwa hekima zao walihisi kuwa bwana Katanga hakuhusika moja kwa moja na
mashtaka hayo. Nadhani waadhiriwa wanafurahia kuwa ofisi yake
inafuatilia suala hili, ili kuhakikisha kuwa mashtaka mazito kama hayo
yanachunguzwa.'' Aliongeza Bensouda.
Kuhusiana na kesi inayomkabili rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, makamu wake William
Ruto na mwandishi wa habari Joshua arap Sang, Bensouda alisema kuwa
''Nimeonyesha wazi kuambatana na ombi niliowasilisha mbele ya mahakama,
kuhusiana na changa moto tunazopata, baada ya mashahidi wakuu kujiondoa
kwa sababu kadhaa''.
Bensouda
amesema kuwa itakuwa vigumu sana kwa ofisi yake kuendelea na kesi hizo
kama ilvyopangwa baada ya mashahidi wakuu kujiondoa.
''Nimewafahamisha
majaji kuwa tulikuwa na mashahidi kadhaa wakuu ambao walikuwa tayari
kutoa ushahidi kuhusiana na matukio muhimu nchini Kenya, lakini wameomba
kujiondoa kutoka kwa kesi hiyo.
Na kama
unavyofahamu mashtaka haya pia ni mazito, na kabla ya kwenda mahakamani
mtu anapaswa kuwa na uhakika wa kuwa na ushahidi ambao utakidhi mahitaji
muhimu ili kuhakisha kuwa washukiwa wanahumiwa.'' Alisema Bensouda.
0 comments:
Post a Comment