Meli inayoidaiwa kutokomea
Bunge la Libya limemuengua madarakani
Waziri Mkuu wa nchi hiyo Ali Zeidan, baada ya vikosi vya nchi hiyo
kushindwa kuzuia kutoroka kwa meli iliyokuwa imebeba shehena ya mafuta
huku ikipeperusha bendera ya
Korea ya Kaskazini. Jumla ya wabunge 124 kati ya 194 waliohudhuria
bungeni Jumanne ya jana waliidhinisha kura ya kutokuwa na imani kwa
wingi wa kura zaidi ya kiwango kinachotakikana na hivyo kuweza kumuondoa
madarakani Waziri Mkuu wa nchi hiyo Ali Zeidan.
Wakati huohuo bunge hilo la Libya
limemteuwa Waziri wa Ulinzi Abdullah al Thani kuwa Waziri Mkuu wa Mpito,
na hivyo bunge hilo kuwa na muda wa wiki mbili wa kutafuta shakhsia
mwingine atakayechukua nafasi ya Zeidan. Itafahamika kuwa, wanamgambo
wanaoidhibiti bandari ya Sedra huko mashariki mwa Libya, Jumamosi wiki
hii walipakia mafuta kwenye meli hiyo iliyokuwa na bendera ya Korea ya Kaskazini kwa jina la "Morning Glory" ambayo ilitia nanga kwenye bandari hiyo bila ya kibali cha serikali.Chanzo, tehranswahili.com
0 comments:
Post a Comment