Ofisi ya
Katibu wa Bunge Maalum inawatangazia Wajumbe wa Bunge Maalum na umma
kwa ujumla kuwa Mkutano wa Bunge Maalum utaendelea mjini Dododma kesho
kwa ratiba ifuatayo:
Tarehe 17/3/201 kuanzia saa 3:00 asubuhi kutakuwa na kiapo kwa Wajumbe wa Bunge Maalum ambao bado hawajaapishwa. Hivyo Wajumbe
wote ambao hawajaapa kiapo cha ujumbe wa Bunge Maalum wanatangaziwa
kufika Idara ya Shughuli za Bunge Maalum kesho saa 2:00 asubuhi bila
kukosa kwa ajili ya kutambuliwa.
Saa 11:00 jioni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba atawasilisha Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum.
Tarehe 18/3/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi Wajumbe wote wa Bunge Maalum watapewa semina kuhusu ufahamu mpana zaidi wa Kanuni za Bunge Maalum.
Tarehe 19 na 20/3/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi wajumbe wote watapewa semina kuhusu Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tarehe
21/3/2014 saa 3:00 asubuhi kutakuwa na uteuzi wa Wajumbe wa Kamati za
Bunge Maalum na saa 10:00 jioni Mgeni Rasmi ambaye ni Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania atalihutubia Bunge kuashiria ufunguzi rasmi wa
Bunge Maalum.
Atakayeipata taarifa hii amjulishe mwenzake.
Imetolewa na Ofisi ya
KATIBU WA BUNGE MAALUM
0 comments:
Post a Comment