Shughuli ya kutafuta ndege ya abiria
ya Malaysia imeendelea kushika kasi baada ya kuwepo kwa hali ya
suitofahamu na wasiwasi mwingi kutoka kwa ndugu za watu waliopotea
wakiwa katika ndege hiyo.
Mamlaka nchini Malaysia zinasema
wameongeza mipaka ya eneo la utafutaji, mara mbili Zaidi, huku China
ikiwa imepeleka mitambo 10 ya satelaiti kwa ajili ya kusaidia kutafuta
ndege hiyo.
Mkuu wa Idara ya anga Azharuddin
AbdulRahman amewaambia waandishi wa habari kuwa eneo la kusaka ndege
hiyo limeongezeka mara mbili kutoka maili 50 za baharini kunakosemekana
ndege ilipotelea mpaka maili 100.
Ndege iliyokua imebeba watu 239
ilipotea bila kutoa taarifa yeyote na hakuna dalili yeyote mpaka sasa ya
kupatikana kwa mabaki ya ndege hiyo
0 comments:
Post a Comment