Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Samwel Sitta akila kiapo mbele ya Katibu
wa Bunge hilo Bw. Yahya Khamis Hamad, wakati wa hafla ya kuwaapisha
wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba jana Mjini Dodoma.Kulia ni Naibu
Katibu wa Bunge Hilo Thomas Kashilila.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samia Suluhu Hassan akila kiapo mbele ya Naibu Katibu wa Bunge Hilo Thomas
Kashilila, wakati wa hafla ya kuwaapisha wajumbe wa Bunge Maalum la
Katiba Mjini Dodoma.Kulia ni Katibu wa Bunge Hilo Yahya Khamis Hamad.
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba na Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda akila kiapo
cha kuwa Mjumbe wa Bunge Hilo Mbele ya Mwenyekiti wa Bunge Hilo Samwel
Sitta.
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba na aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hilo
Pandu Ameir Kificho akila kiapo cha kuwa Mjumbe wa Bunge Hilo Mbele ya
Mwenyekiti wa Bunge Hilo Samwel Sitta.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Edward Lowassa akila kiapo cha kuwa Mjumbe wa Bunge Hilo Mbele ya Mwenyekiti wa Bunge Hilo Samwel Sitta.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye ni Mwanasheria Mkuu Frederick Werema akitoa hoja wakati wa hafla ya kuwaapisha wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma.
0 comments:
Post a Comment