>>NI ‘TOPPS STICKERS’, AMBAZO WATU HUKUSANYA PICHA ZA MASTAA!!
VETERANI Ryan Giggs, ambae sasa ni Kocha-Mchezaji waMabingwa
wa England Manchester United, ametunukiwa Tuzo maalum toka kwa TOPPS,
ambao ndio Wasambazaji rasmi wa Stika za Ligi Kuu England, ambayo
inadhaminiwa na Barclays.
Giggs alipewa zawadi Maalum ya
Kumbukumbu ambayo ina mkusanyiko wa Stika maalum za Misimu yote 21 ya
Ligi Kuu England ambayo yeye ndie Mchezaji pekee kucheza Misimu yote
hiyo.
Kampuni ya TOPPS imekadiria kuwa tangu
Giggs, mwenye Miaka 40, aanze kucheza Ligi Kuu England ilipoanzishwa
Mwaka 1992, ni zaidi ya Nusu Bilioni za Stika zilitengenezwa na kati ya
hizo za Ryan Giggs ni zaidi ya Milioni 7.
Akijiona kwenye Stika hizo za kila Msimu
kwa Misimu 21, Giggs amesema ni furaha kubwa na hasa kujiona kwenye
Jezi tofauti za kila Msimu lakini Jezi ambayo anaikumbuka zaidi ni ile
ya Mwaka 1999 ambapo walitwaa Trebo na Man United, yaani FA CUP, Ubingwa
wa England na UEFA
CHAMPIONZ LIGI.
Giggs amekiri kuwa hivi sasa Wachezaji
wenzake wanamcharura kuhusu Nywele zake ambazo Stika hizo zinaonyesha
zilianza ndefu na nyeusi wakati yu mdogo na sasa zenye mvi na chache.
Nae Chris Rodman, Kiongozi wa TOPPS,
ametamka: “Ryan Giggs amepata mafanikio makubwa kupita Mchezaji yeyote
kwenye Miaka 22 ya Ligi Kuu England. Ametwaa Ubingwa mara 13 na kucheza
Mechi zaidi ya 600. Yeye ndio Mchezaji pekee ambae ametokea kwenye
Matoleo Rasmi ya Stika za Ligi Kuu England kila Msimu.”
0 comments:
Post a Comment