Afisa
Uhusiano wa Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia Simwanza
akizungumza na wanahaabari (hawapo pichani) kuhusu vipodozi vilivyopigwa
marufuku na mamlaka hiyo.Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya
Habari(MAELEZO) Frank Mvungi.
Picha na Husssein Makame-MAELEZO.
Afisa
Uhusiano wa Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia Simwanza,
akionesha moja ya vipodozi vilivyopigwa marufuku na mamalaka hiyo
kinachotumiwa na wanawake kukuza makalio.
Baadhi ya wanahabari wakimsikiliza Afisa Uhusiano wa Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia Simwanza (hawapo pichani).
Picha na Hussein Makame-MAELEZO.
Frank Mvungi-Maelezo
MAMLAKA
ya Chakula na Dawa (TFDA) imeteketeza vipodozi visivyofaa kwa matumizi
ya binadamu vyenye thamani ya takribani Shilingi Milioni 188 katika
kipindi cha mwaka 2012/2013.
Hayo
yamesemwa na Afisa Uhusiano wa mamlaka hiyo, Gaudensia Simwanza wakati
akizunguza na wanahabari kwenye mkutano na waandishi wa habari leo
jijini Dar es salaam.
Alisema
TFDA imeweka mfumo thabiti wa udhibiti wa vipodozi ambao unatumia njia
mbalimbali ambazo ni pamoja na usajili wa vipodozi, utoaji wa vibali vya
biashara ya bidhaa husika na ukaguzi wa majengo ya vipodozi.
Simwanza
aliongeza kuwa hatua nyingine ni ufuatiliaji wa vipodozi katika soko
ili kujiridhisha kuwa vina ubora na usalama unaotakiwa kwa mujibu wa
sheria na taratibu zilizowekwa.
Alibainisha
kuwa vipodozi ambavyo havifai kwa matumizi ya binadamu vina madhara
kama vile kusababisha kupata mzio wa ngozi, kusababisha ugonjwa wa ngozi
kwa mtumiaji.
“Matumizi
ya vipodozi vyenye viambata vya zebaki (mercury) kwa mama wajawazito
huathiri mtoto tumboni hali inayoweza kusababisha madhara makubwa kwa
mtoto atakayezaliwa.
Alifafanua
zaidi kuwa viambato kama Zirconium na Vinyl Chloride husababisha kansa
ya ngozi na mapafu kwa mtumiaji wa vipodozi vyenye kemikali.
Simwanza alitoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kwa kuacha matumizi ya vipodozi vyenye viambata vyenye sumu na kemikali.
TFDA
imekuwa ikifanya operesheni na ukaguzi wa vipodizi katika maduka
mbalimbali yanayouza bidhaa hizo na kukamata bidhaa zisizofaa kwa
matumizi ya binadamu na kuziteketeza kwa mujibu wa sheria.
0 comments:
Post a Comment