Tuesday, 11 March 2014

RATIBA VPL YAREKEBISHWA, LIGI KUMALIZIKA APRILI 19!!

>>DABI YA KARIAKOO: YANGA v SIMBA APRILI 19!!
>>MTIHANI WA MAWAKALA WA WACHEZAJI APRILI 3
>>22 KUSHIRIKI SEMINA YA WAAMUZI DAR
SOMA ZAIDI:
Release No. 042
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Machi 11, 2014
22 KUSHIRIKI SEMINA YA WAAMUZI DAR
UWANJA_WA_TAIFA_DARWaamuzi na waamuzi wasaidizi 22 wameteuliwa kushiriki semina na mtihani wa utimamu wa mwili kwa robo ya kwanza ya mwaka huu itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Machi 14 hadi 16.
Semina hiyo inashirikisha waamuzi wote wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na wale wa ngazi ya juu (elite) kutoka Tanzania Bara za Zanzibar.
Waamuzi hao ni Charles Simon (Dodoma), Dalila Jafari (Zanzibar), Ferdinand Chacha (Mwanza), Hamis Chang’walu (Dar es Salaam), Helen Mduma (Dar es Salaam), Israel Mujuni (Dar es Salaam), Issa Vuai (Zanzibar), Janeth Balama (Iringa), Jesse Erasmo (Morogoro), John Kanyenye (Mbeya) na Jonesia Rukyaa (Bukoba).
Josephat Bulali (Zanzibar), Lulu Mushi (Dar es Salaam), Martin Saanya (Morogoro), Mfaume Nassoro (Zanzibar), Mohamed Mkono (Tanga), Mwanahija Makame (Zanzibar), Ngaza Kinduli (Zanzibar), Oden Mbaga (Dar es Salaam), Ramadhan Ibada (Zanzibar), Samwel Mpenzu (Arusha) na Waziri Sheha (Zanzibar).
Wakufunzi wa semina hiyo ambao wanatambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ni Joan Minja na Riziki Majala.

RATIBA VPL YAREKEBISHWA, LIGI KUMALIZIKA APRILI 19
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeifanyia marekebisho ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ambapo sasa itamalizika Aprili 19 mwaka huu badala ya Aprili 27 mwaka huu.
Marekebisho hayo yamefanyika ili kutoa fursa kwa timu ya Taifa (Taifa Stars) kujiandaa kwa mechi za mchujo la Kombe la Afrika 2015 ambapo itacheza raundi ya awali Mei mwaka huu.
Kutokana na marekebisho hayo, Yanga itacheza na Prisons (Uwanja wa Taifa) Machi 26 mwaka huu katika mechi ya raundi ya 17 wakati Machi 19 mwaka huu kwenye uwanja huo huo ni Yanga na Azam.
Machi 15 mwaka huu kutakuwa na mechi mbili; Azam na Coastal (Azam Complex), na Mtibwa Sugar itacheza na Yanga (Jamhuri). Mgambo na Azam zitacheza Machi 26 mwaka huu Mkwakwani, na Aprili 9 mwaka huu Yanga itaialika Kagera Sugar (Taifa).
Raundi ya 22 itaanza Machi 22 mwaka huu kwa mechi kati ya Kagera vs Prisons (Kaitaba), JKT Ruvu vs Mbeya City (Azam Complex), na Rhino vs Yanga (Ali Hassan Mwinyi). Machi 23 mwaka huu ni Simba vs Coastal (Taifa), Mgambo vs Mtibwa (Mkwakwani), Ruvu Shooting vs Ashanti (Mabatini) na Azam vs Oljoro (Azam Complex).
Machi 29 mwaka huu itaanza raundi ya 23 kwa mechi kati ya Ashanti vs Oljoro (Azam Complex) wakati Machi 30 ni Mbeya City vs Prisons (Sokoine), Kagera vs Ruvu Shooting (Kaitaba), Mtibwa vs Coastal (Manungu), JKT Ruvu vs Rhino (Azam Complex), Azam vs Simba (Taifa), na Mgambo vs Yanga (Mkwakwani).
Raundi ya 24 inaanza Aprili 5 mwaka huu kwa Kagera vs Simba (Kaitaba), Ashanti vs Mbeya City (Azam Complex). Aprili 6 mwaka huu ni Coastal vs Mgambo (Mkwakwani), Oljoro vs Prisons (Sheikh Kaluta Amri Abeid), Rhino vs Mtibwa (Ali Hassan Mwinyi), Ruvu Shooting vs Azam (Mabatini) na Yanga vs JKT Ruvu (Taifa).
Aprili 12 mwaka huu inaanza raundi ya 25 kwa Mtibwa vs Ruvu Shooting (Mabatini), Coastal vs JKT Ruvu (Mkwakwani), Prisons vs Rhino (Sokoine). Aprili 13 mwaka huu ni Mgambo vs Kagera (Mkwakwani), Simba vs Ashanti (Taifa), Mbeya City vs Azam (Sokoine) na Oljoro vs Yanga (Sheikh Kaluta Amri Abeid).
Raundi ya 26 ni Aprili 19 mwaka huu kwa Rhino vs Ruvu Shooting (Ali Hassan Mwinyi), Mbeya City vs Mgambo (Sokoine), Prisons vs Ashanti (Jamhuri, Morogoro), JKT Ruvu vs Azam (Azam Complex), Oljoro vs Mtibwa (Sheikh Kaluta Amri Abeid), Coastal vs Kagera (Mkwakwani) na Yanga vs Simba (Taifa).

MTIHANI WA MAWAKALA WA WACHEZAJI APRILI 3
Mtihani kwa ajili ya watu wanaotaka kuwa mawakala wa wachezaji wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Aprili 3 mwaka huu saa 4 kamili asubuhi ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (FIFA).
Kwa wanaotaka uwakala huo wanatakiwa kujisajili ambapo watapewa kanuni mbalimbali za FIFA na TFF ili waweze kujiandaa kikamilifu kwa mtihani huo utakaokuwa na sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ya mtihani huo ni maswali kutoka FIFA wakati nyingine ni kutoka TFF.
Tanzania ina mawakala watatu tu wa wachezaji wanaotambuliwa na FIFA. Mawakala hao ni Ally Saleh, John Ndumbaro na Mehdi Remtulla.
Boniface Wambura Mgoyo
Media and Communications Officer
Tanzania Football Federation (TFF)

0 comments: