Saturday, 15 March 2014

LIGI KUU ENGLAND: MAN CITY YAPANDA, IPO NAFASI YA 2 BAADA YA KUICHAPA HULL CITY 2-0

>>NAHODHA KOMPANY KADI NYEKUNDU, KUZIKOSA FULHAM, MAN UNITED & ARSENAL!

MANCHESTER City imerudi nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Hull City jioni hii.
Ikitoka kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na Barcelona, timu ya Manuel Pellegrini leo ilipania kubeba pointi tatu katika Ligi Kuu na shukrani kwao wafungaji wa mabao hayo, David Silva dakika ya 14 na Edin Dzeko dakika ya 90. Lakini City ilimaliza pungufu baada ya Nahodha wake, Vincent Kompany kutolewa nje kwa nyekundu dakika ya 10 baada ya kumchezea rafu mshambuliaji wa Hull City, Nikica Jelavic. 
Na kwa ushindi huo,City inatimiza pointi 60 baada ya kucheza mechi 27 na kurejea nafasi ya pili, nyuma ya Chelsea yenye pointi 66 baada ya mechi 29. 

Wote pamoja: Wachezaji wa City wakishangilia ushindi wao leoMarching orders: Vincent Kompany shows his disbelief after being shown a straight red by referee Lee Mason
Marching orders: Vincent Kompany shows his disbelief after being shown a straight red by referee Lee Mason
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumapili Machi 16
1630 Man United v Liverpool
1900 Tottenham v Arsenal

MSIMAMO:
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Chelsea
29
34
66
2
Man City
27
44
60
3
Liverpool
28
38
59
4
Arsenal
28
24
59
5
Tottenham
29
0
53
6
Man United
28
12
48
7
Everton
27
11
48
8
Newcastle
28
-2
43
9
Southampton
30
2
42
10
West Ham
28
-4
31
11
Aston Villa
28
-7
31
12
Stoke
29
-14
31
13
Hull
29
-7
30
14
Swansea
28
-4
29
15
Norwich
29
-22
29
16
Crystal Palace
28
-19
27
17
West Brom
28
-11
25
19
Cardiff
29
-28
25
18
Sunderland
26
-16
24
20
Fulham
29
-36
21

0 comments: