Wiki moja tangu ndege ya Malaysia iliyokuwa imewabeba abiria 239 kutoweka, juhudi za kimataifa kuisaka ndege hiyo bado zinaendelea.
Mataifa
kumi na mbili sasa yamejiunga pamoja kuisaidia serikali ya Malaysia na
msako huo, juhudi zenyewe zikijikita zaidi Magharibi mwa rasi ya
Malaysia.(Hudugu)
Marekani
imesema kuwa inatuma manowari zake za kivita, pamoja na ndege maalum ya
uchunguzi katika maeneo ya Bengal, Bahari ya Andaman na sehemu za Bahari
hindi.
Mnamo
Ijumaa taarifa ziliibuka kuwa ndege hiyo ilituma mawasiliano katika
kituo cha trafiki ya ndege kwa karibu saa tano baada ya taarifa ya
kupotea kwake kutolewa.
Taarifa
zinasema kuwa mawasiliano hayo yanaweza kusaidia katika kujua iliko
ndege hiyo na ndio maana Marekani ikaamua kutuma meli zake za kivita
katika Bahari Hindi.CHANZO BBC
0 comments:
Post a Comment