MSHAMBULIAJI Lionel Messi
amefunga mabao matatu katika ushindi wa 7-0 wa Barcelona dhidi ya
Osasuna Uwanja wa Camp Nou kwenye mchezo wa La Liga jioni hii.
Messi
sasa anaweka rekodi nyingine kwa hat-trick hiyo, akiwa mfungaji bora wa
kihistoria Barcelona kwenye mashindano yote, baada ya kufikisha mabao
371 akimpiku Paulino Alcantara.
Messi pia sasa amebakiza bao moja kumfikia gwiji wa zamani wa Real Madrid, Hugo Sanchez
kwa ufungaji bora kwenye historia ya La Liga. Anaweza kumpiku Sanchez
wiki ijayo katika dhidi ya mahasimu, Real Madrid Uwanja wa Santiago
Bernabeu.
Juu ya chati: Lionel Messi akisherehekea baada ya kuweka rekodi mpya
Heshima: Ujumbe unaoonyesha salamu za pongezi kwa Messi baada ya kuweka rekodi mpya Barcelona
Muargentina
huyo alifungua biashara leo dakika ya 18 akimalizia pasi ya Alexis
Sanchez ambaye alifunga la pili dakika ya 22 kwa pasi ya Jordi Alba
kabla ya Andres Iniesta kufunga la tatu dakika ya 34 kwa pasi ya Sergio
Busquets.
Kipindi
cha pili, Messi tena alifungua biashara dakika ya 63 kwa pasi ya
Iniesta aliyetoa pia na pasi ya bao la tano lililofungwa na Tello dakika
ya 78.
Messi
akaurudisha mpira nyavuni tena dakika ya 88 kukamilisha hat trick yake
kwa pasi ya Dani Alves kabla ya kutoa pasi ya bao la saba kwa Pedro
dakika ya 90.
Barcleona sasa inabaki inazidiwa pointi nne Real Madrid katika mbio za ubingwa La Liga.
Tutaonana siku nyingine: Messi akiondoka na mpira wake bada ya mechi
Messi akiwapangua wachezaji wa Osasuna Uwanja wa Nou Camp
0 comments:
Post a Comment