Sunday, 16 March 2014

ALIBINO ATIWA MBARONI KWA KUMCHUNA NGOZI MTOTO SEHEMU YAKE YA SIRI

DSC001791
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida SACP, Geofrey Kamwela.
Na Nathaniel Limu, Singida
MKULIMA mkazi wa kijiji cha Nkalankala kata ya Mwanga,tarafa ya Nduguti wilaya ya Mkalama mkoani Singida ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino) ,Hidaya Omari (20),anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kumnyonga hadi kufa, mtoto wake wa kiume mwenye umri wa mwaka moja na nusu,na kisha kumchuna ngozi katika sehemu yake ya siri.
Mtoto aliyenyongwa na kuchunwa ngozi ya sehemu yake  ya siri na kutupwa kwenye kisima cha maji chenye kina cha mita moja,ni Richard Paulo.
Imedaiwa pia mama yake mzazi na mtuhumiwa Hidaya,Neema Paulo (35), naye anashikiliwa na polisi kwa tuhuma ya kuhusika  kumnyonga Daudi Richard na kumsababishia kifo.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida,SACP,Geofrey Kamwela,alisema tukio hilo la kusikitisha,limetokea machi 13 mwaka huu saa moja na nusu asubuhi huko katika kijiji cha Nkalankala wilayani Mkalama.
Alisema mtoto huyo Daudi,aliokotwa akiwa anaelea juu ya maji ya kisima chenye urefu wa mita moja.
Kamwela alisema uchunguzi wa awali wa jeshi la polisi,umebaini kuwa Daudi (marehemu) aliuawa na kuchunwa ngozi yake na kutumbukizwa katika kisima hicho.
Alisema mwili wa marehemu ulipofanyiwa uchunguzi na daktari katika eneo la tukio na kubaini kuwa kabla ya mauaji jhayo,mtoto huyo alinyongwa shingo yake.Chanzo cha mauaji hayo,inasadikiwa kuwa ni imani ya kishirikina.
Kamanda Kamwela alisema mara upelelezi utakapokamilika,watuhumiwa mtu na mama yake,watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.

0 comments: