Afisa wa kijeshi wa Marekani
Maafisa
wa Marekani wanaosaidia kaisaka ndege ya Malyasia iliyotoweka Jumamosi
iliyopita, wanasema kuwa taarifa mpya sasa inawaelekeza hadi Magharibi
mwa bahari ya Hindi.
Vyombo
vya habari nchini Marekani vinasema kuwa huenda ndege hiyo ilikuwa
ikituma data katika mtambo wa setllite kwa muda wa masaa manne baada ya
kutoweka kutoka katika mitambo ya rada ikiwa njiani kuelekea Beijing.
Wanajeshi wa majini wa Marekani imetuma meli iliyo na Helikopta kadhaa hadi katika eneo mpya ndani ya bahari ya Hindi.
Maafisa
wa serikali ya Marekani wameiambia shirika la habari la ABC kuwa vitengo
viwili vya mawasiliano katika ndege iliyopotea ilikwama kuwasilisha
data kwa muda tofauti, kumaanisha kuwa janga baya halikutokea.
0 comments:
Post a Comment