>>AGOMA KUOMBA RADHI NA KUPIGWA FAINI YA 'QUENELLE'!!
KLABU ya West Bromwich Albion
imetangaza kumufukuza Straika wao Nicolas Anelka kwa Utovu wa Nidhamu
wakati Straika huyo ambae amefungiwa na FA Mechi 5 alitangaza Jana kuwa
anaondoka mwenyewe Klabu hiyo.
Jana Anelka, mwenye Miaka 35, aliandika
kwenye Mtandao wake kuwa anaondoka Klabuni hapo baada kushindwa
kuridhiana kufuatia Kifungo cha Mechi 5 na kupigwa ya Faini £80,000 na
FA, Chama cha Soka England, kwa kutoa Saluti ya 'quenelle' Uwanjani
ambayo ilichukuliwa kama ni ya Kibaguzi.
Nayo WBA ikajibu mapigo kwa tamko la
Anelka kwa kutangaza kumfukuza kwa Utovu wa Nidhamu kwa kumpa Notisi ya
Siku 14 ya kufutwa kazi.
Akiandika Mtandaoni, Anelka alisema:
“Kufuatia Majadiliano kati ya Klabu na mimi, masharti fulani yaliwekwa
ili mie nirudi kwenye Timu, ambayo sikuyakubali. Ili kubakisha utu
wangu, nimevunja Mkataba na West Brom mara moja.”
Hata hivyo, West Brom ilichukulia hatua
hiyo kuwa ni Utovu wa Nidhamu na kutoa Taarifa ilisema: “Uvunjwaji
Mkataba si wa haki kwa sababu umefanywa nje ya Sheria.”
Klabi hiyo pia ilianika masharti ambayo
Anelka alitakiwa kufanya ili aendelee kubaki hapo ambayo ni kuomba
radhi, kwa Mashabiki, Wafadhili na Umma kwa jumla kuhusu Saluti ya
'quenelle' aliyoitoa Uwanjani Desemba 28 na pia akubali kutwangwa Faini.
Mkataba wa Anelka na WBA ulitakiwa
umalizike mwishoni mwa Msimu na kufuatia Kifungo chake cha Mechi 5,
Anelka angeweza kucheza tu Mechi 5 za mwisho za Msimu huu.
Sakata la Anelka lilianza Desemba 28 wakati akishangilia Goli lake Timu yake, West Bromwich Albion, ilipotoka Sare 3-3 na West Ham, kwa kutumia ishara ya Saluti ambayo inahusishwa na Mafashisti wa Nazi.
Saluti hiyo [Pichani] ambayo Mkono wake
wa kushoto aliupitisha Kifuani na Mkono wa Kulia kuelekezwa chini
huchukuliwa kama Saluti ya Nazi kwa kinyume lakini mwenyewe Anelka
amekiri hiyo inaitwa ‘Quenelle’ ili kumsapoti Rafiki yake wa France,
Dieudonné M'Bala M'Bala, ambae ni Mchekeshaji, anaesakamwa Nchini humo
kwa kuwa Mbaguzi.
Saluti hiyo ya Anelka imezua kizaazaa
kikubwa huko Ufaransa kiasi ambacho Waziri wa Michezo Nchini humo,
Valérie Fourneyron, amesema inatia kinyaa.
Anelka alitumia hiyo ‘Quenelle’
akisheherekea Bao lake la Kwanza kati ya mawili iliyofunga kwenye Sare
hiyo ya 3-3 kati ya Timu yake West Brom na West Ham na hilo likiwa Bao
lake la Kwanza kwa Klabu hiyo tangu ajiunge nayo mwanzoni mwa Msimu.
0 comments:
Post a Comment