>>AITAJA BAYERN TIMU NZURI LAKINI MSIMU HUU NI DHAIFU!
>>ROBBEN AJIBU: ‘ÚKIWA MENEJA MKUBWA KUBALI KUFUNGWA! ACHA KULALAMIKA MAMBO YA KIPUUZI!’
MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger amembatiza Fowadi wa Bayern Munich Arjen Robben
kuwa ni ‘Mwangukaji Stadi’ kufuatia Jana Sare ya Bao 1-1 kati ya Bayern
na Arsenal ambayo iliwatupa nje ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, Timu hiyo
ya England.
Arsenal wametolewa nje ya UCL kwa
kufungwa Jumla ya Mabao 3-1 baada kufungwa 2-0 huko London Mwezi
uliopita katika Mechi ya Kwanza na sasa Bayern Munich, ambao ndio Mabingwa Watetezi wa Kombe hili, wanatinga Robo Fainali.
Hiyo Jana huko Allianz Arena, Munich, Bayern walitangulia kufunga kwa Bao la Bastian Schweinsteiger
na Arsenal kusawazisha kupitia Lukas Podolski na pia kunusurika
kufungwa kwa Penati ya Dakika za Majeruhi ambayo ilipigwa na Thomas
Muller na kuokolewa Kipa Lukasz Fabianski ambae alikuwa Golini kuchukua
nafasi ya Wojciech Szczesny aliepewa Kadi Nyekundu kwa kumchezea vibaya
Arjen Robben katika Mechi ya Kwanza na hivyo kufungiwa Mechi hii.
Robben ndie aliesababisha Penati hiyo
‘laini’ ya Jana iliyokoswa na Thomas Muller baada kuanguka
alipokabiliana na Sentahafu wa Arsenal, Laurent Koscielny.
Mapema Kipindi cha Pili, huku
akikabiliwa na Santi Cazorla, Robben alijiangusha lakini Refa kutoka
Norway, Svein Oddvar Moen, hakutoa Penati lakini pia hakumpa Kadi ya
Njano Robben kwa kujiangusha.
Akikumbusha pia tukio la Robben la Mechi
ya Kwanza aliposababisha Kipa Wojciech Szczesny kupewa Kadi Nyekundu na
kutolewa Penati, Wenger alifoka: “Robben ni mzuri sana katika kupata
mengi bila kuwepo kitu. Ni Mchezaji mzuri na pia mwangukaji mzuri! Yeye
hukatiza mbele ya Mtu na kupunguza kasi na kujiangusha. Anapata frikiki.
Ndio maana Jana tuliongea kuhusu Marefa. Kama Refa angempa Kadi kwa
tukio la kwanza lile la pili lisingetokea!”
Wenger pia alisema tofauti yao na Bayern
ilikuwa kwenye Mechi ya Kwanza na kile kilicholeta tofauti ni Kadi
Nyekundu kwa Kipa Wojciech Szczesny.
Wenger aliwatakia heri Bayern na kusema: “Nawatakia heri Bayern, ni Timu nzuri lakini Msimu huu wapo dhaifu kupita Mwaka Jana.”
Nae Arjen Robben amejibu mapigo kwa
kusema: “Siku zote nimesema ukiwa Meneja mkubwa kubali kufungwa.
Ukishinda, furahia na ustarehe lakini ukifungwa acha kulalamika mambo ya
kipuuzi!”
0 comments:
Post a Comment