Saturday, 15 March 2014

UCHAGUZI SIMBA SC MEI 4, KASSIM DEWJI AREJESHWA MSIMBAZI

Na Dina Ismail, Dar es Salaam
KIKAO cha Kamati ya Utendaji ya Simba SC kilichomalizika mida hii mjini Dar es Salaam, kimepanga Mei 4,mwaka huu iwe tarahe ya Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo, imeelzwa.

Ofisa Habari wa Simba SC, Asha Muhaji ameuambia mtandao huu   leo kwamba kikao hicho pia kimeunda Kamati ya Uchaguzi chini ya Mwenyekiti Damas Ndumbaro na Makamu wake, Salum Madenge.
Wanachama wa Simba SC wanatangaziwa Uchaguzi Mkuu Mei 4 mwaka huu

Wengine katika Kamati hiyo ni Issa Batenga ambaye ni Katibu, Khalid Kamguna Katibu Msaidizi na Wajumbe Kassim Dewji, Juma Simba na Amin Bakhresa.

Kesho Simba SC inatarajiwa kufanya mkutano wa wanachama wake kwa ajili ya kuifanyia marekebisho Katiba yao kwa maagizo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

0 comments: