Kamati ya PAC Leo imekutana na Benki Kuu ya Tanzania kupokea Maelezo kuhusu fedha tshs 201 bilioni za akaunti ya Tegeta Escrow.
Fedha hizi zinahusiana na mkataba IPTL. PAC ina wasiwasi kwamba
TANESCO, kwa mujibu wa nyaraka, itatakiwa kulipa fedha nyingi zaidi
zinazofikia zaidi ya tshs 200 bilioni kwa kampuni iliyonunua IPTL.
Kamati imeamua kwamba;
1)
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali afanya ukaguzi maalumu wa
suala zima IPTL na uhalali wa utoaji wa fedha kutoka akaunti maalumu ya
tegeta escrow.2)
TAKUKURU waanze uchunguzi wa mchakato mzima wa mkataba wa IPTL, umiliki
wa kampuni hiyo na uhamishaji wa umiliki kwenda kampuni ya PAP.
Kamati imeshangazwa na kitendo
cha Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini kuanzisha ukaguzi maalumu
wakati yeye mwenyewe ni mtia saini kwenye hati ya kutoa fedha hizo na
mshiriki mkubwa katika mchakato mzima. Hivyo, kamati imeagiza ukaguzi
maalumu kutoka kamati PAC ili kuweza kupata ukweli.
PAC
imetoa mpaka mwisho wa mwezi Aprili kwa taarifa ya ukaguzi huo kuwa
umekamilika na kuwataka wahusika wote wa mchakato wa IPTL kusubiri
matokeo ya ukaguzi.
PAC imetaka pia maamuzi ya mahakama kuheshimiwa.
Imetolewa na Mwenyekiti PAC-Zitto Kabwe(MB)
Dodoma
Jumapili 16 Mechi 2014
0 comments:
Post a Comment