“PRESS RELEASE” TAREHE 13.03.2014.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAWASHIKILIA WATU WATANO KWA TUHUMA ZA MAKOSA MBALIMBALI KUTOKANA NA MISAKO ILIYOFANYIKA
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAWASHIKILIA WATU WATANO [05] KWA TUHUMA ZA MAKOSA MBALIMBALI KUTOKANA NA MISAKO ILIYOFANYIKA.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATANO [05] KUHUSIANA NA
TUHUMA ZA MAKOSA MBALIMBALI. KATIKA TUKIO LA KWANZA ALPHONCE PATRICK
[19] MKAZI WA KIJIJI CHA MBALA WILAYA YA CHUNYA ALIKAMATWA AKIWA NA
BHANGI KETE 10 ZENYE UZITO WA GRAM 50. TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE
11.03.2014 MAJIRA YA SAA 15:13 ALASIRI KATIKA KIJIJI CHA MBALA, KATA YA
MBALA, TARAFA YA KWIMBA KUFUATIA MSAKO ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI.
AIDHA
WATU WENGINE WAWILI 1.KILLY SHUSHA [18] NA 2. MLAWA SAKSON [18] WOTE
WAKAZI WA KIJIJI CHA MAGAMBA WILAYA YA CHUNYA WALIKAMATWA NA JESHI LA
POLISI WAKIWA NA BHANGI GRAM KUMI [10]. TUKIO AMBALO LILITOKEA TAREHE
12.03.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI KATIKA KIJIJI NA KATA YA
MAGAMBA, TARAFA YA SONGWE, KUFUATIA MSAKO ULIOFANYWA NA JESHI LA
POLISI.
KATIKA
TUKIO JINGINE WATU WAWILI 1. CHAZALI INYAMAGOHA [45] NA 2. SAMWEL
MTOKOMA [50] WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA ISONGOLE WILAYA YA ILEJE
WALIKAMATWA WAKIWA NA MALI IDHANIWAYO KUWA YA WIZI. CHAZALI INYAMAGOHA
ALIKAMATWA AKIWA NA MIFUKO MINNE [04] YA SIMENTI NA SAMWEL MTOKOMA
ALIKAMATWA AKIWA NA NONDO 55 MALI INAYODHANIWA KUWA NI YA WIZI KUTOKA
KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI YA VODACOM. TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE
12.03.2014 MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI KATIKA KIJIJI HICHO CHA ISONGOLE
TARAFA YA BULAMBYA, KUFUATIA DORIA /MSAKO ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA
KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
AIDHA ANATOA RAI KWA JAMII KUACHA TAMAA YA UTAJIRI WA HARAKA KWA
KUTUMIA NJIA ZA MKATO KWANI HUWEZI KUPAMBANA NA UMASIKINI WA KIPATO KWA
NJIA ZA MKATO BADALA YAKE WANANCHI WAFANYE KAZI HALALI KWA LENGO LA
KUPATA KIPATO HALALI IKIWA NI PAMOJA NA KUNUNUA MALI HALALI KATIKA
SEHEMU HUSIKA. PIA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA ANATOA WITO KWA
WANANCHI KUENDELEA KUTOA TAARIFA SAHIHI NA KWA WAKATI KUHUSIANA NA
UHALIFU NA WAHALIFU ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI
YAO.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment