Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu Damian Lubuva akifafanua jambo kwa msisitizo kuhusia na maandalizi
ya mwisho ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, unaotarajiwa kufanyika
Machi 16, mkutano huo umewakutanisha wadau mbalimbali vikiwemo vyama
vya Siasa,vyombo vya usalama na wadau wengine
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu Damian Lubuva akizungumza
mbele ya waandishi wa habari mapema leo,kuhusu uchaguzi mdogo wa jimbo
la Kalenga katika kikao cha pamoja na vyama vilivyosimamisha wagombea
kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo ulioko
Halmashauri ya wilaya ya Iringa Vijijini.Uchaguzi wa Jimbo hilo
unatarajiwa kufanyika Machi 16.Ambapo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi
ameeleza kuwa idadi ya wapiga kura jumla yao ni 71,765.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu Damian Lubuva akijadiliana
jambo na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu
Hamid Mahmoud Hamid kwenye mkutano uliohusu kupeana taarifa ya
maandalizi ya mwisho ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga,unaotarajiwa
kufanyika Machi 16,mkutano huo umewakutanisha wadau mbalimbali vikiwemo
vyama vya Siasa,vyombo vya usalama na wadau wengine,mkutano huo
umefanyika leo asubuhi kwenye ukumbi wa Siasa ni Kilimo zilizomo ndani
ya Ofisi za Halmashauri Wilaya ya Iringa.
Mkurugenzi
wa Oparesheni wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) katika
uchaguzi wa Kalenga,Benson Kigaila wakisalimiana kwa furaha na Mmratibu
wa kampeni CCM Kalenga Miraji Mtaturu.
Mkurugenzi
wa Oparesheni wa chama cha demokrasia na maendeleo katika uchaguzi wa
Kalenga Benson Kigaila aliyesimama kwa nyuma akizungumza na mratibu wa
kampeni ccm Kalenga Miraj Mtaturu kulia kwake ni mratibu wa uchaguzi wa
ccm Taifa Edwin Millinga.
Kamanda
wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi akijadiliana
jambo na Afisa msajili msaidizi wa vyama vya siasa Sisty Nyahoza.
Wanahabari wakijadiliana jambo.
Baadhi ya Wanahabari wakiwa katika kikao cha Tume ya Uchaguzi n Vyama vya siasa na baadhi ya wadau wa usalama.
PICHA NA MICHZUIJR. MICHUZI MEDIA GROUP-IRNGA
0 comments:
Post a Comment