MAHAKAMA ya huko Ujerumani imemhukumu Kifungo Rais wa Mabingwa wa Ulaya Bayern Munich, Uli Hoeness, kwa ukwepaji kulipa Kodi.
Hoeness, licha ya kuungama mwenyewe
kwamba alikwepa Kodi, Mahakama hiyo haikumwonea huruma na kuamua kumpa
Kifungo cha Miaka Mitatu na Nusu Jela.
Jaji wa Mahakama, Rupert Heindi, aliamua
kuwa kuungama kwa Hoeness kulikuwa na kasoro na pia hakutimiza matakwa
ambayo yangempa Msamaha wa Kifungo.
Hoeness alikiri kukwepa Kodi ya Euro Milioni 27.2 ambayo alipaswa kulipa kufuatia kuwa na Akaunti kwenye Benki ya Uswisi.
Hoeness, mwenye Miaka 62 na ambaye akiwa
kama Mchezaji aliisaidia Ujerumani Magharibi kutwaa Kombe la Dunia
Mwaka 1974 na kama Kiongozi wa Bayern aliinua sana Klabu hiyo Kiuchumi
na Kimafanikio, aliondoka Mahakamani bila kuzungumza na Wanahabari.
Hata hivyo, Mawakili wake wamesema watakata Rufaa Mahakama ya Juu huko Germany.
Huko Germany, ukwepaji kulipa Kodi ni
kosa kubwa na huvuna Kifungo cha Juu cha Miaka 10 lakini kwenye Kesi ya
Uli Hoeness, Waendesha Mashitaka walitaka afungwe Miaka 5 na Nusu kwa
vile alikiri na kuisaidia Mahakama.
Awali Hoeness alishitakiwa kwa kukwepa
Kodi ya Euro Milioni 3.5 lakini Kesi ilipoanza Jumatatu hii, Hoeness
aliistua Mahakama kwa kukubali kuwa alikwepa Kodi ya Euro Milioni 18.5
na hii iliongezeka na kufikia Euro Milioni 27.2 Siku ya Pili ya
kusikilizwa Kesi kufuatia ushahidi wa Inspekta wa Kodi.
Hadi sasa haijulikani kama Hoeness atabaki kuwa Kiongozo wa Bayern Munich na Klabu hiyo imesema itajadili suala hilo.
Bayern Munich inamilikiwa Kibinafsi
lakini Kampuni kubwa za Germany, Adidas AG, Allianz na Audi AG, kila
moja inamiliki Hisa za Asilimia 8.3 kila moja huku Deutsche Telekom AG
wakiwa ndio Wadhamini wakubwa.
0 comments:
Post a Comment