Taarifa ambazo zimethibitishwa na tovuti ya
Yanga kuhusu kunusurika ajali bus walilokuwa wakisafiria kutoka
Morogoro kurudi Dar baada ya kumalizika kwa mchezo kati yao na Mtibwa Sugar ya Manungu Morogoro mechi ambayo ilimalizika kwa suluhu ya 0-0.
Wakati wanarudi asubuhi ya leo Bus la timu yao ambayo lilikuwa
limebeba wachezaji pamoja na viongozi wa benchi la ufundi limepata ajali
eneo na Mikese Mizani baada ya Mabus yaliyokua yakitanua kuelekea mikoa
ya bara kuziba njia na kusababisha kutumbukia kwenye mtaro.
Katika
ajali hiyo iliyotokea majira ya saa tatu na nusu asubuhi hakuna mtu
yeyote aliyejeruhiwa na kwa sasa timu inaondoka na usafiri wa bus
jingine kuelekea jijini Dar es salaam
Basi la Yanga likiwa limeinama upande mmoja baada ya kukwepa basi la abiria. Hakuna aliyeumia na timu imeendelea na safari ya kurejea Dar es Salaam baada ya mkasa huo |
0 comments:
Post a Comment