Aliyekuwa waziri mkuu wa Libya, Ali
Zeidan, amepuuzilia mbali kura ya kutokuwa na imani naye iliyotangazwa
na Bunge la taifa hilo mapema juma hili iliyopeleekea kufutwa kwake.
Ameiambia shirika la habari la Channel
France 24 kuwa kura hiyo ya kutokuwa na imani naye illikuwa imejengwa
kwa misingi ya uwongo huku pia akikanusha madai ya ufisadi dhidi ya
serikali yake.
Ali Zeidan aliondolewa Ofisini mnamo
siku ya Jumanne baada ya meli ya mafuta kutoka bandari inayodhibitiwa na
waasi kufaulu kuvunja nanga ya wanajeshi wa wanamaji wa Libya kuingia
bahari kuu na kutoroka.
Bwana Zeidan alifaullu kuondoka nchi hiyo licha ya kupingwa marufuku ya kutosafiri nje ya taifa
0 comments:
Post a Comment