.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara 
wa kumnadi mgombea wa CCM, Silaa alisema hawana budi kuichagua CCM kwa 
sababu ndiyo iliyoshika dola kwa miaka mitano 2010-2015.
Alisema kama wananchi wa kijiji hicho na jimbo kwa ujumla wanataka maendeleo ya haraka, lazima waiunge mkono CCM kwa kumchagua Godfrey Mgimwa.
"Wananchi wa Kijiji cha Mgama na jimbo lote,
 kama mnataka maendeleo kwa haraka ni lazima muichague CCM na siyo chama
 kingine kwa sababu Serikali iliyopo madarakani ni ya CCM," alisema 
Silaa.
Naye mwenyekiti wa CCM Tawi la Ihemi, 
Greyson Mlowe alimtaka mgombea ubunge katika jimbo hilo kutatua 
changamoto ya maji katika kata ambapo wabunge waliopita walijaribu 
kuitatua bila ya mafanikio.
Alisema yeye ni mzaliwa wa Kata ya 
Mgama kwa muda mrefu , kuna baadhi ya viongozi wamekwenda kuomba kura, 
lakini walipopata walipotea na kuwaacha wakihangaika na changamoto zao.
Naye Mgimwa alisema atashirikiana na 
viongozi wa nyanja mbalimbali kuhakikisha anatatua changamoto za 
wananchi wa jimbo hilo endapo watamchagua.
Alisema kuwa kutokana na changamoto 
nyingi za wananchi hao, ameamua kutumia elimu aliyonayo ili aweze 
kuzifikisha kwa viongozi mbalimbali na kupatiwa ufumbuzi.
Uchaguzi huo utafanyika Jumapili ijayo
 






 
 
 
 






0 comments:
Post a Comment