Mpira ni mchezo unaogusa hisia za watu wengi zaidi Duniani. Ipo michezo mingi, lakini unapozungumzia soka unagusa mamilioni ya watu kuliko mchezo wowote unaoujua.
Wapo mashabiki wengi ambao kila muda wanajadili soka. Hata hapa Tanzania,
ukipita kwenye vijiwe mbalimbali, baa, ofisi za watu na maeneo mengi
ambayo watu wanakutana kupiga gumzo, hawaachi kuzungumzia kabumbu.
Nchini
Tanzania, klabu za Simba na Yanga zina wapenzi wengi zaidi ya klabu
yoyote. Unapotaja klabu hizi, unagusa hisia za Watanzania wengi.
Ndio maana kwenye mechi zao, ni rahisi kwa watu kuzirai au kupoteza fahamu pale matokeo mabaya yanapoikumba timu moja.
Kama
inafika wakati watu wanapoteza fahamu baada ya timu zao kufungwa na
wengine kuamua kujiua, utagundua kuwa timu hizi zina mvuto mkubwa kwa
mashabiki wake.
Kama
mtu anaweza kukumbwa na matatizo hayo ya kiafya kwasababu timu
imefungwa, lazima uwe makini unapopewa dhamana ya kuogoza klabu hizi.
Kuwa
kiongozi wa Simba na Yanga, kunahitaji uwe na uelewe mkubwa wa kutambua
kuwa nyuma yako kuna watu wengi wenye mapenzi ya dhati na timu zao.
Unapoleta mchezo na mambo muhimu yanayohusu klabu, unawaumiza watu bila sababu ya msingi.
Nirudi kwenye hoja yangu ya msingi iliyonisukuma kuandika makala hii.
Kesho machi 16 klabu ya Simba itafanya mkutano wa wanachama wake kwa ajili ya kuifanyia marekebisho Katiba yao.
Na Baraka Mpenja wa Dar es salaam
0712461976 au 0764302956
Kusoma zaidi bofya hapa chini
0 comments:
Post a Comment