KIKOSI cha Yanga SC kinaondoka usiku mjini Cairo kurejea Dar es Salaam
baada ya kutolewa katika Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika na
mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri Jumapili kwa penalti 4-3 baada ya
sare ya jumla ya 1-1.
Ahly
ilishinda 1-0 juzi baada ya dakika 90 Uwanja wa Border Guard (Haras
Hodoud) na kufanya sare ya jumla ya 1-1 kutokana na Yanga pia kushinda
1-0 katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam na katika mikwaju ya penalti
wakashinda 4-3.
Yanga ilitua jana Cairo ikitokea Alexandria
na kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa wapinzani wao, Al Ahly kabla ya
kualikwa chakula cha jioni kwa Balozi wa Tanzania nchini hapa, Mohammed
Hamza.
Yanga SC ambao ni mabingwa wa Bara wamekubali matokeo na wanarejea Tanzania
kuelekeza nguvu zao katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ili
watetee ubingwa wao, ambako wanatarajiwa kutua majira ya Saa 12:00
asubuhi.
Kocha
Mkuu wa klabu hiyo, Mhoalnzi Hans Van der Pluijm alisema kwamba vigogo
wa Misri Al Ahly wamepoteza makali yao na si timu tisho tena ile
aliyokuwa anaijua yeye, licha ya kuitoa timu yake juzi kwa penalti mjini
Alexandria.
“Ilivyo,
Al Ahly hii si timu kali tena ambayo sote tulikuwa tunaijua na ikiwa
wataendelea kucheza kama hivi katika hatua ijayo, nina uhakika
watataabika,”.
“Tulikuwa
karibu kuwatoa nje ya mashindano, lakini penalti ni mchezo wa bahati,
na ninajivunia kiwango chetu,”alisema Pluijm baada ya mechi juzi.
Baada
ya kuitoa Yanga SC, timu hiyo yenye maskani yake mjini Cairo itakutana
na Al Ahly Benghazi kuwania kuingia Hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Yanga
SC ambayo katika Ligi Kuu ya Bara inakabiliwa na ushindani mkali kutoka
kwa Azam FC katika mbio za ubingwa, itamenyana na Mtibwa Sugar Uwanja
wa Jamhuri, Morogoro Jumamosi.
Yanga SC inashika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu kwa pointi zake 38 kutokana na mechi 17, nyuma ya Mbeya City yenye pointi 39, baada ya kucheza mechi 21, wakati Azam ipo kileleni kwa ponti zake 40 baada ya mechi 18
Na Salum Esry, Cairo
BIN ZUBARRY BLOG
0 comments:
Post a Comment