Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
0712461976 au 0764302956
MCHEZAJI nyota wa Asernal, Alex Oxlade-Chamberlain anaamini kuwa klabu yake itasonga mbele katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya (UEFA Champions League)
katika mchezo ya marudiano hapo kesho, licha ya kupigwa mabao 2-0 na
mabingwa watetezi, Bayern Munich mchezo wa kwanza uwanja wa Emirates
jijini London.
Kiungo
huyo amejenga imai hiyo kwa kutumia uzoefu wa msimu uliopita ambapo
washika bunduki hao walishinda mabao 2-0 katika dimba la Allianz Arena
baada ya kupoteza mchezo wa kwanza katika dimba lao kwa mabao 3-1,
hivyo anaamini kwa asilimia 100 kuwa kitu hicho kinaweza kujirudia.
Asernal
wapo katika furaha ya kuwabamiza Everton mabao 4-1 katika mchezo wa
kombe la FA na kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ambapo
watakabiliana na Wigan uwanja wa Wembley, hivyo kuwa na matumaini ya kutwaa kombe la kwanza tangu mwaka 2005.
Alex Oxlade-Chamberlain akipanda ndege wakati wakielekea uwanja wa Luton Airport jijini Munich nchini Ujerumani
Mchezo
wa marudiano utakaopigwa kesho utaamua hatima ya Asernal katika
michuano ya kimataifa barani Ulaya. Kama watatupwa nje basi watabaki
katika kinyang`anyiro cha ubingwa wa ligi kuu nchini England ambapo wapo
katika ratiba ngumu ya kuwavaa ugenini Tottenham na Chelsea kabla ya
kuwakaribisha nyumbani, Manchester City machi 29.
Bayern Munich
wameweka rekodi katika ligi ya Bundesliga baada ya kushinda michezo 16
mfululizo na mchezo wa mwisho waliwafunga mabao 6-1 Wolfsburg, na sasa
kikosi cha Pep Guardiola kipo mbele kwa pointi 20 dhidi ya wapinzani wao
wa karibu, Borussia Dortmund huku wakibakiwa na mechi 10.
Asernal
watamkosa kiungo wao, Muingereza Jack Wilshere ambaye yupo nje kwa wiki
sita baada ya kuvunjika mguu, wakati huo huo mlinda mlango wao namba
moja. Wojciech Szczesny ataukosa mchezo huo kufuatia kuoneshwa kadi
nyekundu katika mchezo wa kwanza.
Mholanza,
Oxlade-Chamberlain alisisitiza kuwa bado nafasi ipo kama Asernal
wataendeleza rekodi ya ushindi wa mabao 2-0 katika dimba la Allianz
Arena, msimu wa mwaka jana. Kikubwa watafute mabao tu.
Tayari kwa safari: Mesut Ozil, Mathieu Flamini na Lukas Podolski wakielekea uwanja wa ndege
Kazi tu: Mathieu Flamini na Laurent Koscielny wakiwa ndani ya ndege kuelekea Munich
“Nsdiyo,
asilimia 100 tunaweza kushinda. Msimu uliopita tulifungwa 3-1
nyumbani-kila mtu aliona hatuwezi, lakini tuliweza kuwafunga kwao 2-0″.
Alisema kiungo huyo.
“Tutaweza kufanya vizuri ukizingatia tulicheza kwa kiwango cha juu jumamosi dhidi ya Everton”.
Katika soka, vitu vingi vinaweza kutokea. Tunajua wanajua kazi haijaisha, hata sisi tunajua kazi haijaisha”. Aliongeza.
Kazi imenza: Wachezaji wa Arsenal, Mesut Ozil na Lukas Podolski wakiwasili mazoezi huku wakionekana hawana wasiwasi.
Wagumu wa ngome: Per Mertesacker na Laurent Koscielny wakiwasili katika mazoezi ya kuwakabili Bayern Munich
Wachezaji wa Arsenal wakipasha jijini London katika dimba la Colney kabla ya kuwasili Munich
0 comments:
Post a Comment