MKURUGENZI wa Manispaa
ya Moshi mkoani Kilimanjaro Bernadeta Kinabo,ametelekeze agizo la baraza la
madiwani la kumtaka kuvunja nyumba iliyojengwa katika eneo la wazi bila kibali
kuvunjwa.
MTANDAU HUU imefika katika eneo la tukio leo asubuhi na kushuhudia shughuli ya
kuvunja nyumba hiyo ikiwa ikekwisha fanyika ambapo baadhi ya mashuhuda walisema
tukio hilo lilitokea majira ya saa 7:00 usiku.
Nyumba hiyo inayolalamikiwa na madiwani hao kujengwa katika eneo la
wazi ipo katika mtaa wa “Police Mess” barabara ya Mawenzi karibu na makao makuu
ya Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro.
Katika baraza la madiwani lililo kaa juzi katika ukumbi wa Manispaa
mkurugenzi huyo alitakiwa kuvunja nyumba hiyo pamoja na baadhi ya nyumba
nyingine zilizo jengwa kinyume cha sheria.
Diwani wa kata ya Kiusa Steven Ngasa amedai katika kikao hicho kuwa
nyumba hiyo ilijengwa kinyume cha sheri na kwamba madiwani wamekuwa wakilaumiwa
kuchukua rushwa kutoka kwa wamiliki hao jambo ambalo si kweli.
Alisema kuwa kumekuwa na ujenzi holela unaoendelea ndani ya manispaa hiyo
huku watendaji wa Halmashauri hiyo wakiwa hawatambukii chochote kinacho endelea
jambo ambalo ni uzembe.
“tabia hii ya ujenzi holela imekuwa ikishamiri siku hadi siku na mbaya zaidi
wanakiuka sheria jambo hili hatuta livumili kuona linaendela katika manispaa
yetu”Alisema
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa Kinabo alisema kuwa baadhi
ya madiwa wamekuwa wakipita kwa wamiliki wa majengo hayo huku wakichukua rushwa
jambo ambalo limekuwa likikwamisha shughuli hizo kuendelea.
Naye Meya wa manispaa hiyo Jafari Michael aliwataka madiwani kuacha tabia
ya kuwa “mawakala wa nyumba” na kutanguliza maslahi mbele kwani wao ndio chanzo
cha migororo inayo endelea ndani ya mansipaa hiyo.
Akizungumzia tukio la kuvunjiwa nyumba yake, mmiliki wa Nyumba hiyo, John Ambrose Mwase amesema hapo mwanzoni alikuwa anafanya biashara ya mgahawa katika eneo hilo kabla ya kuiomba manispaa imbadilishie leseni ya biashara na kibali cha kufanya biashara tofauti katika eneo hilo.
Amesema anashangazwa kusikia kuwa ujenzi wa nyumba hiyo umefanyika bila
kibali na kuhoji ni kwa nini manispaa ichukue uamuzi wa kuvunja majira ya usiku
na kuharibu mali bila taarifa.
Mwasi amesema leseni alipewa na Afisa biashara wa manispaa ambaye pia
alifika na kukagua eneo hilo kabla ya ujenzi kuanza. ameongeza kuwa gharama
aliyotumia kujenga nyumba hiyo ambayo ni mkopo wa benki ya KCB ni kubwa mno
ambayo ni sh milioni 85 pamoja na nyingine za kuendeshea biashara ambazo ni sh.
milioni 165.
Mwandishi: KIJA ELIAS, Moshi-Kilimanjaro
0 comments:
Post a Comment