Tunaomba radhi kwa picha zitakazo onekana
Rukia
Haruna (31) akitolewa nje na Askari wa Jeshi la Polisi akitolewa nje
ya Mahakama kwenda Gerezani kutumikia kifungo cha miaka 5 Jela
****************************
HIVI NDIVYO ILIVYO KUWA JUNI 14 .2013 ENEO LA MANGA A JIJINI MBEYA
*********************
Mwanamke mmoja mkazi wa Manga A Jijini Mbeya
amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa kosa la kutupa mtoto wake chooni.
Tukio hilo lilitokea Juni 14,
Mwaka huu katika eneo hilo baada ya watoto waliokuwa wakicheza kugundua kuwepo
kwa Mtoto katika choo cha shimo.
Mtuhumiwa baada ya kukamatwa
amekiri kutenda kosa hilo na kwamba alifanya hivyo baada ya mzazi mwenzie
kumkataa.
Ameongeza kuwa amelazimika
kutupa katika choo cha jirani kwa sababu ni cha shimo tofauti na chao ambacho
asingeweza kutupa mtoto huyo.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali,
Archiles Mulisa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Zabibu
Mpangula, amemtaja Mtuhumiwa kuwa ni Rukia Haruna (31) mkazi wa Manga A Jijini
Mbeya na kwamba kosa lake ni kinyume cha kifungu 218 kifungu kidogo cha 35 sura ya 16 ya mwaka
2002.
chanzo Mbeya yetu
0 comments:
Post a Comment