MWENYEKITI
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kata ya Sungaji, wilaya
ya Mvomero, mkoani Morogoro, amemtaka Naibu Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Amos Makala, kujiuzulu kwa kushindwa kudhibiti
wafugaji.
Mwenyekiti
wa CHADEMA kata hiyo, Musa Kombo, amesema Makala pamoja na baadhi ya
viongozi wa mkoa na wilaya wameshindwa kuwachukulia hatua wavamizi
(wafugaji) ambao wameharibu kiasi kikubwa cha mashamba na kusababisha
njaa.
Kombo alitoa
kauli hiyo mara baada ya kumalizika kwa mkutano uliofanyika katika
kijiji cha Kigugu Julai 11.7 na kuhutubiwa na Naibu Waziri huyo.
Makala katika hali iliyowashangaza wengi, alijibu kiwepesi sana maswali yaliyoulizwa na wananchi.
Katika
majibu yake kuhusiana na uvamizi wa wafugaji, Makalla alisema yeye ni
kama mwananchi mwingine wa kawaida na kwamba suala la wafugaji ni gumu
hata Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ameshindwa kutoa Suluhu.
Kiongozi huyo wa CHADEMA alisema kuwa majibu kama hayo, yamewakatisha mno tamaa wakulima wanaoitegemea serikali kuwasaidia.
“Wakulima
wanapopewa majibu mepesi kwa maswali magumu, wanahisi hawana viongozi wa
serikali wanaomsaidia Rais, na kudhani hana watu wa kumsaidia kujibu
hoja za msingi,” alisema.
Mbali ya
swali la mgogoro wa wakulima na wafugaji, maswali mengine ambayo Makala
alishindwa kutoa majibu ni kuhusu fedha za Mfuko wa Jimbo, wakati lile
la ahadi yake ya ujenzi wa zahanati alisema anangoja kwanza aone juhudi
za wananchi ndipo atawasaidia na pia kufuatia mradi wa maji (PADEP)
ambao unasuasua hakutoa jibu la kuridhisha zaidi ya kuwakatisha tamaa
wananchi.
Majibu hayo
pia yalimsononesha Katibu wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Sungaji Shukuru
Mikenegeze aliyesema, “Kama ulivyomsikia mbunge, wafugaji wana nguvu ya
fedha, hivyo itabidi na sisi tuanzishe vikundi vya kijamii kulinda
mazao yetu yasiharibiwe na mifugo, jambo ambalo watu wanadai itaibuka
vita.
0 comments:
Post a Comment