Kiungo wa klabu ya Arsenal na
timu ya taifa ya Ujerumani Mesut Ozil amesema miaka ijayo anaamini
atashinda tuzo ya Ballon d’or na jinsi wachambuzi wanavyozidi kumkosoa
ndiyo anapata nguvu ya kujituma zaidi.
Mjerumani huyo ameichezea Arsenal
mechi 14 tu katika ligi kuu msimu huu kufuatia kukaa nje ya uwanja kwa
muda mrefu akiuguza majeraha lakini tangu arudi tena uwanjani amekuwa
katika kiwango bora.
Mchezaji huyo aliyesajiliwa msimu
uliopita akitokea Real Madrid anaonekana kuizoea ligi ya Uingereza
tofauti na hapo awali. “Nikiendelea kufanya vizuri, afya yangu ikawa
imara basi miaka michache ijayo Ballon d’or itakuwa mikononi mwangu”
alisema Ozil. .”Ninajisikia vizuri. Mimi ni mchezaji mkubwa
duniani,ninacheza katika klabu kubwa. Pia hii ligi tunatumia nguvu
nyingi kuliko kule La Liga kwa hiyo ninazidi kuimarika zaidi kuliko
mwanzo ” aliongeza Ozil.
Pia mchezaji huyo amesema kitendo
cha kiungo wa zamani wa Manchester United Paul Scholes kuponda kiwango
chake kilimuongezea nguvu ya kupambana na kuongeza kujituma zaidi.
Ozil sasa yupo katika majukumu ya
timu ya taifa ya Ujerumani ambao jumapili watashuka dimbani kuwavaa
Georgia katika mechi ya kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya mataifa
Ulaya yatakayofanyika mwaka 2016 nchini Ufaransa.
0 comments:
Post a Comment