POLISI mkoani Mwanza inashikilia risasi
277 zilizookotwa vichakani na raia wema katika eneo la Lumala, wilayani Ilemela
mkoani hapa.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu alisema
juzi walipokea taarifa kutoka eneo hilo kuwa zimeokotwa risasi 277 za silaha ya kivita aina ya SMG.
Kwa
mujibu wa Kamanda, risasi hizo zilitupwa katika eneo hilo na zilikutwa kwenye
galoni ya lita tano baada ya kuokotwa na raia wema.
Inasadikiwa
zilitupwa na wahalifu ambao jeshi hilo bado linaendelea kuwasaka katika
operesheni yake inayoendelea kwenye wilaya za Sengerema, Kwimba na Magu.
operesheni yake inayoendelea kwenye wilaya za Sengerema, Kwimba na Magu.
Kamanda
Mangu amezihusisha risasi hizo na majambazi mawili waliouawa wiki iliyopita
wakati wakirushiana risasi na polisi walipotaka kufanya uporaji katika duka la
wakala wa Kampuni ya Bia (TBL) katika eneo la Igoma.
“Itakumbukwa
kuwa Mei 18, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi waliwaua majambazi
wawili waliojaribu kufanya uporaji eneo la Igoma ambao walikuwa na silaha aina
ya SMG,” alisema Kamanda Mangu.
Alisema
baadaye ilifahamika kuwa majambazi hao walikuwa ni wahalifu sugu ambapo
waliwahi kukamatwa wakiwa na risasi 597 za SMG kisha kufungwa jela.
CHANZO: HABARILEO
0 comments:
Post a Comment