Monday, 27 May 2013

KEZI YA UPORAJI WA MIL 239 ZA NMB KUTOLEWA JUNE 4

Hukumu kesi ya uporaji wa Sh239 mil za NMB sasa kutolewa Juni 4

 

 


Moshi. 
Usikilizwaji wa kesi ya wizi wa Sh239 mali ya Benki ya NMB, Tawi la Mwanga sasa umefikia ukingoni baada ya jopo la mahakimu watatu kupanga Juni 4 kuwa siku ya kutoa hukumu.
Kesi hiyo inawakabili raia wawili wa Kenya, Samwel Saitoti na Peter Kimani na Watanzania watano wanaotuhumiwa kuvamia benki hiyo Julai 2007 na kupora fedha hizo chini ya mtutu wa bunduki.
Katika uporaji huo, polisi mmoja wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) aliyekuwa lindo aliuawa.
Jopo hilo la Mahakimu waandamizi watatu, Pantrine Kente, Aziza Temu na John Nkwabi wamepanga tarehe hiyo baada ya mawakili wa pande zote mbili kukamilisha uwasilishaji wa majumuisho.
Tarehe ya kutolewa kwa hukumu hiyo inayovuta hisia za wananchi wengi ndani na nje ya Mji wa Moshi ilitangazwa wiki iliyopita na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Simon Kobelo wakati akiahirisha kesi hiyo.


Na Daniel Mjema, Mwananchi gazeti

0 comments: