Saturday, 18 May 2013

RAIS JAKAYA KIKETE ATEMBELEA KIWANDA CHA EAST COAST OILS & FATS



Rais Jakaya Mrisho Kikwete  alitembelea kiwanda cha EAST COAST OILS & FATS
Jana Mei 17, 2013, Rais Jakaya Mrisho Kikwete  alitembelea kiwanda cha EAST COAST OILS & FATS ambacho ni kampuni tanzu ya MeTL kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam ili kuhamasisha jishe bora kwa walaji kwa kuongezaji Virutubishi vya Vitamini A katika Vyakula vinavyozalishwa viwandani yakiwemo mafuta ya kupikia.
Picture
Pichani ni Mheshimiwa Rais Kikwete akimimina mafuta ya virutubishi katika kinu cha kutengeneza mafuta ikiwa ni ishara ya uzinduzi  wa kampeni hiyo.

Wanaoshihudia tukio hilo pichani juu, ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq (kushoto), Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL Bw. Vijay Raghavan ( wa pili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya MeTL Mh. Mohammed Dewji (Mb) (wa tatu kushoto) pamoja na wadau wengine wa masuala ya Lishe.
 

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya MeTL Mh. Mohammed Dewji (Mb) wakati wakisubiri kuwasili kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipotembelea Kampuni ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL kuhamasisha Lishe Bora kwa walaji kwa kuongezaji Virutubishi vya Vitamini A katika Vyakula vinavyozalishwa viwandani yakiwemo mafuta ya kupikia. 
(Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog).


Picha juu na chini Viongozi mbalimbali wa Serikali na Wafanyakazi wa Kiwanda ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL wakisubiri kumpokea Rais.


Wafanyakazi wa Kiwanda ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL wakisubiri mkumpokea Rais.


Dewji (Mb), akimlaki Rais Kikwete mara baada ya kuwasili.



Afisa Mwajiri wa kampuni ya East Coasts Oils and Fats ambayo ni Kampuni tanzu ya MeTL Bw. Eric Buberwa akisalimana na Rais.


Rais Kikwete akiendelea kusalimiana na wadau mbalimbali wa masuala ya Lishe.


Dewji (Mb), akiteta jambo na Rais wakati wakielekea sehemu ya kiwanda cha East Coasts Oils and Fats. Kushoto ni Said Meck Sadiq.


Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL Bw. Vijay Raghavan akifafanua jambo kwa Rais Kikwete kabla ya kukumimina iirutubishi vya Vitamini A katika kinu cha kuzalisha mafuta kiwandani hapo ikiwa ni ishara ya kuhamasisha lishe bora kwa walaji.


Vijay Raghavan akitoa maelezo kwa Rais na Mkewe, ya namna wanavyopima mafuta yao kwa teknolojia ya kompyuta.


Dewji (Mb) akifafanua jambo kwa Rais Kikwete.


Rais Kikwete akiwahutubia wafanyakazi wa Kampuni ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL mara baada ya kumaliza zoezi la kutembelea kampuni hiyo inayozalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo mafuta ambapo amempongeza Mh. Mohammed Dewji kwa kutengeneza ajira kubwa kwa Watanzania kupitia kiwanda chake.


Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL wakimsikiliza Rais.


Picha ya pamoja ya Rais, Mkewe, wageni waalikwa, Uongozi wa Kampuni ya MeTL pamoja na wadau wa masuala ya lishe alipotembelea Kiwanda cha East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL katika kampeni ya uongezaji wa virutubishi vya Vitamini A katika vyakula vinavyozalishwa viwandani.


Rais akizungumza na Dewji (Mb) (kushoto) mara baada ya kuhutubia wafanyakazi. Wa pili kushoto ni Said Meck Sadiq na mdau wa masuala ya lishe.


Dewji (Mb), akiagana na Rais Kikwete

 

0 comments: