HATIMAYE
wasamaria wameanza kujitokeza katika kumsaidia mtoto Joshua Joseph ambaye
alifungiwa ndani zaidi ya miaka miwili huku akikosa matunzo muhimu na kupelekea
mtoto kupata ugonjwa wa utapia mlo.
Moja ya Wasamaria hao Familia ya mama Masawe toka DSM wametoa magodoro mawili, nguo,mashuka,chakula
pamoja na lishe ya mtoto.
Akipokea
msaada huo jana, ofisa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamiii, Habiba Ibrahimu
alisema wasamaria hao wameonyesha uzalendo na kuokoa maisha ya mtoto
ambayo kwa asilimia kubwa yalikuwa hatarini.
Aidha,
Daktari wa kituo cha Afya, Inyala kilichopo Kata ya Iyunga, Queen Mwakijambile,
alisema baada ya vipimo kufanyika mtoto huyo amekutwa na tatizo la utapiamlo
huku uzito wa mwili ukiwa haulingani na umri wake.
“Baada
ya mtoto Joshua kufikishwa kwenye kituo hiki cha matibabu na kufanyiwa vipimo,
tumebaini mtoto alikosa lishe pamoja na uzito wake kufikia kilo nane
ukilinganisha na umri wake wa miaka miwili,”alisema
Alisema,
uzito wa kilo nane ulipaswa kuwa na mtoto wa miezi sita au saba hivyo hatua
aliyofikia alikuwa kwenye hatari ya kupoteza uhai wake.
Naye
Balozi wa Mtaa wa Ikuti Aron Mboya, aliwashukuru wasamaria hao na kwamba
serikali ya kijiji itasimimia na kuhakikisha mtoto huyo anapata huduma zote za
kiafya pamoja na kumsimamia mama mlezi kutumia misaada hiyo kwa malengo
yaliyokusudiwa kwa mtoto huyo.
(picha zote na mbeya yetu)
0 comments:
Post a Comment