Waziri Mkuu alitembelea Ofisi ya CCM Mtwara
Vijijini, Mahakama ya Mwanzo ya Mitengo, Ofisi ya Kata ya Mtonya
Mikindani, Ofisi ndogo ya Mbunge (Murji), Baa ya Mukuzi, nyumba ya
Mwenyekiti wa CCM Mkoa na ya Mbunge wa Mtwara Vijijini.Mtwara. Mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnain Murji ameikacha
ziara ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokuwa akitembelea maeneo
yaliyoathiriwa na vurugu zilizotokea mkoani hapa wiki iliyopita.
Katika ziara yake, Waziri Mkuu alitembelea Ofisi
ya CCM Mtwara Vijijini, Mahakama ya Mwanzo ya Mitengo, Ofisi ya Kata ya
Mtonya Mikindani, Ofisi ndogo ya Mbunge (Murji), Baa ya Mukuzi, nyumba
ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa na Nyumba ya Mbunge wa Mtwara Vijijini, ambaye
pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia
ambazo zilishambuliwa katika vurugu za mwanzo.
Akizungumzia sababu za kukacha ziara hiyo, Murji
alisema: “Ni kweli nilialikwa lakini kilichonifanya nisiungane na Waziri
Mkuu ni ratiba kutokuonyesha kutembelea maeneo ya wananchi waliopatwa
na maafa.
“Ratiba ile ilionyesha Waziri Mkuu atatembelea
maeneo ya viongozi na Mahakama pekee bila kutembelea maeneo ya wananchi
ndiyo sababu iliyonifanya nisihudhurie, wananchi wasingenielewa.
Wangenigeuka na wangeniona nimewasaliti.
“Kwa kuwa nipo upande wa wananchi, nisingeweza
kutembelea maeneo ya viongozi wa Serikali pekee lakini kesho (leo)
wakati Waziri Mkuu akitembelea walioathirika na mimi nikiwa Mbunge wa
Mtwara Mjini nitatembelea maeneo yote ya wananchi wangu waliokumbwa
zahama hiyo.”
Murji alisema sababu ya kukataa gesi isitoke ni
kutokana na nafasi nyingi za ajira kupatiwa wananchi wa nje kwa asilimia
90 huku asilimia 10 pekee ikibaki kwa wananchi wa Mtwara hali
inayowafanya wananchi wasijue ni nini kitakachofuata baada ya gesi
kupelekwa Dar es Salaam.
“Ni kweli wawekezaji ni wengi wanataka kuwekeza
Mtwara na kama tulivyoelezwa kuna maombi ya wawekezaji 45, viwanda vingi
vitakuja lakini ukiangalia upande wa ajira asilimia 90 zote zimeenda
kwa watu wa nje,” alisema Murji.
Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu aliambatana na Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia, wakuu wa wilaya za mkoa huo,
Kamishna wa Polisi (Operesheni), Paul Chagonja, Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Mtwara, Mohamed Sinani na baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Akitoa maelezo ya tathmini ya mali zilizoungua
Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mtonya, Yusuph Kaliwanje alimweleza
Waziri Mkuu kuwa uchomaji wa majengo hayo ulianza saa nane mchana.
Alisema ofisi ya kata hiyo yenye thamani ya Sh32 milioni, ilichomwa moto
pamoja na nyaraka mbalimbali na samani.
Pia alisema vibanda mbalimbali vya wafanyabiashara
pamoja na mali zilizoharibiwa zina thamani ya Sh33 milioni. Alisema
tathmini ya hasara ya Ofisi ya Mbunge bado haijajulikana.
Na Haika Kimaro na Mary Sanyiwa, Mwananchi gazeti
0 comments:
Post a Comment