Baraza la mitihani Tanzania NECTA
limetangaza rasmi matokeo ya Kidato cha Nne 2012. Idadi ya watahiniwa
waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya
asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya
marekebisho alama za viwango vya ufaulu.
Matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa,
ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka
asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia
asilimia 57.
Hii inamaanisha kwamba watahiniwa
wapatao 82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya
awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.
Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka
2012 watakuwa wamefanya vizuri kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa
225,126 sawa na asilimia 53.37 ya 349,390 waliofanya mtihani huo
walifaulu.
Matokeo ya awali yaliyotangazwa na
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa yalionyesha
kuwa kati ya watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani wa kidato cha nne
mwaka jana, waliokuwa wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu
walikuwa 126,847 sawa na asilimia 6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa
ni 103,327 sawa na asilimia 28.1.
Katika matokeo hayo, watahiniwa
240,909 sawa na asilimia 65.5 walipata sifuri, hesabu ambayo imebadilika
katika matokeo mapya ambayo yanaonyesha kuwa sasa waliopata daraja hilo
ni 158,100 ambayo ni asilimia 43.
0 comments:
Post a Comment