Sunday, 19 May 2013

BREAKING NEWS..............MACHAFUKO MAKUBWA IRINGA MACHINGA WAFANYA VURUGU FFU WATUMIA MABOMU

BREAKING NEWS..............MACHAFUKO MAKUBWA IRINGA MACHINGA WAFANYA VURUGU FFU WATUMIA MABOMU

 Polisi  wakipita  eneo la Mashine  tatu asubuhi  hii
 Abiria  na  wapiga  debe  stendi kuu  wakinawa maji baada ya  kupigwa mabomu na kumwagiwa maji ya kuwasha  na askari  wa FFU leo
 Mmiliki  wa mtandao huu mzee wa matukio  daima akinawa maji baada ya  kupigwa  bomu la machozi

 Hali  ikiendelea  kuwa  tete  kwa machinga  kufunga barabara  kuu  ya  Iringa  Dodoma na ile ya mashine  tatu
Ni Machafuko  Iringa  hivi  leo



Mungu ibariki Iringa ,Mungu  wabariki  viongozi  wa  umma mkoani Iringa , Mungu uwape hekima na  busara  viongozi na  machinga  katika  eneo la Mashine  tatu  ili kuepusha madhara ambayo yanazuilika .
Nimelazimika  kuanza  kwa  maneno  hayo  juu  kutokana  na  hali  ilivyo  kwa  sasa katika  jimbo la Iringa  mjini ambapo kumekuwepo na mvutano  usio na tija na mvutano ambao  unaweza  kusababisha madhara makubwa  kwa  siku ya  leo katika  mji  wa Iringa.
Binafsi kama  ni miongoni  wa  watu  wapenda amani na utulivu  nimepatwa na  wakati mugumu  zaidi  baada ya  kauli  ya mbunge mchungaji  Peter Msigwa aliyoitoa juzi katika mkutano  wake  wa hadhara  na  kuirudia  jana katika kipindi maalum radio Nuru Fm ambacho  nilipata  kuendesha baada ya  kusisitiza msimamo  wake  wa  kuwataka Machinga  kuvunja sheria kwa  kufanya biashara  eneo hilo la mashine tatu ambalo kisheria limekuwa  likipigwa marufuku.
Mbunge  Msigwa ambaye  amedai kuwa  leo ataongoza  machinga  kufanyabiashara  katika  eneo  hilo wakati  uongozi  wa Manispaa ya  Iringa  chini ya mstahiki meya  ukisema kuwa  eneo  hilo kisheria halipaswi kufanyiwa  biashara  za umachinga ni wazi  kuwa  huu ni mvutano mkali.
Kama  haitoshi jeshi  la  polisi mkoa  wa Iringa  limepanga  askari  wake  wa  kikosi  cha kutuliza ghasia katika  eneo  hilo ambao  usiku  kuja  wamelala  hapo  kulinda amani na  kuzuia  wale  wote ambao  watajaribu  kuvunja  sheria.
Mtandao  huu  wa    kama chimbuko la amani nchini na duniani  unawaomba  viongozi hawa  kwa maana ya  mbunge, Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa na Machinga kukutana  pamoja na  kuangalia eneo  jingine  la  kufanyia  biashara  machinga  hao ambao hawataki kwenda  eneo la Mlandege ambalo  wamepangiwa na manispaa.
Kwani  haya majibizano na tambo  zinazoendelea  kufanyika sasa  si nzuri  na zinaweza  kusababisha machafuko iwapo hakutakuwa  na kiongozi atakayekubali  kujishusha .
Kama  hoja  ni  machinga  kuwepo mjini  basi  itazamwe  vizuri  hoja  yao  hiyo na ikiwezekana  kuwapa  eneo la uwanja  wa Mwembetogwa  ambao umekuwa  ukitumiwa  kwa  mikutano ya  dini ama  kuwapa  eneo la barabara  mbili kuelekea eneo la uwanja  wa Mwembetogwa hadi shule ya Sekondari Mwembetogwa .
Kama  hapo hapatoshi  basi kuwapa barabara ya  kutoka Parisi  kwenda Veta kupitia  msikiti  wa Hidaya ama  kuwapa eneo la  kuanzia  uwanja  wa Mwembetogwa  kwenda Ilala hadi Msikiti  wa Ilala na  magari  yatumie barabara  ya kwenda  mkwawa na Pawaga  itumike  ile ya Ofisi ya  mkuu  wa mkoa  ambayo inaanzia  eneo la Posta na kwenda  kutokea eneo la Msikiti  wa Ilala .
Kama  itashindikana  kabisa  basi machinga  wapewe  barabara ya Uhindini ama ile ya Legeza mwendo inayoelekea  Kitanzini ambayo  kimsingi haina  msongamano  wa magari na kama haitumiki kabisa.
Wakati  viongozi  wakiendelea  kuvutana machinga  ambao  ndio  wahitaji  wakuu  wa  eneo rafiki  wamempongeza mbunge Msigwa kwa  kuwapigania na  kuwa ila  leo  hawatakuwa tayari  kupanga  bidhaa zao  eneo la Mashine  tatu hadi  atakapopanga  bidhaa zake  Mbunge  wao  huyo na iwapo ataruhusiwa  kuendelea  na biashara  bila  kusumbuliwa na polisi basi na  wao  ndipo  watakapopanga bidhaa zao.

0 comments: