KATIBU Mtendaji wa Baraza la Habari
Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga, ameiomba Serikali iangalie uwezekano wa
kuchukua hatua za ziada za kuwahakikishia waandishi wa habari usalama wawapo
kazini.
Mukajanga
alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumzia vurugu za masuala ya gesi zilizoibuka
wiki iliyopita mkoani Mtwara.
Alisema
MCT inasikitishwa na kilichojiri mkoani humo hasa wananchi kupoteza maisha,
mali kuharibiwa vibaya na amani kutoweka huku maisha ya baadhi ya waandishi wa
habari yakiwa hatarini.
Alisema
baraza hilo lilizungumza na waandishi wa habari wa magazeti ya Serikali ya
Dailynews na HabariLeo yanayomilikiwa na Kampuni ya Standard Newspapers (TSN)
Ltd, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Uhuru na Mzalendo ambao katika
vurugu hizo pamoja na kuharibiwa mali zao walilazimika kukimbilia mafichoni
kuokoa maisha yao.
Aliwataka
wananchi kutambua kwamba kazi ya uandishi wa habari ina misingi yake.
“Jamani
si kila kitu kinaandikwa au ni habari sasa hawa walishambuliwa eti kwa sababu
tu hawakufanya yale ambayo wananchi wanayataka hii si sahihi, mbona mkulima wa
karanga akilima mahindi hashambuliwi kwa kufanya tofauti.”
Aliiomba
Serikali iweke utaribu mzuri wa kuhakikishia waandishi wa habari wanakuwa
salama wanapokuwa kazini huku akisisitizia wamiliki wa habari nao kuwa makini
na matamshi wanayotoa ili kutoweka rehani maisha ya waandishi.
0 comments:
Post a Comment