Thursday, 16 May 2013

KINANA AMKACHA DK SLAA

 
Imeandikwa kwenye gazeti la TANZANIA DAIMA: KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amemkacha Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa.

Wawili hao walitarajiwa kukutana kwenye kipindi kipya kiitwacho ‘Uzalendo’, kinachotarajiwa kuanza kurushwa wakati wowote kuanzia mwezi ujao katika kituo cha televisheni cha ITV.

Taarifa za Kinana kumkimbia Dk. Slaa katika mdahalo huo zilisambazwa jana katika mitandao mbalimbali ya kijamii nchini.

Taarifa hiyo na vyanzo vyetu vingine vya habari, vilieleza kuwa viongozi hao walialikwa na ITV kwa ajili ya mdahalo ambao ungerekodiwa na baadaye kurushwa na kituo hicho.

Kwa mujibu wa habari hizo, viongozi hao walipewa mwaliko wa kuhudhuria kipindi hicho siku kumi zilizopita na wote kuthibitisha ushiriki wao, lakini Dk. Slaa jana alifika katika studio za kituo hicho na kukutana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, badala ya Kinana.

Akizungumza kwa simu na gazeti hili jana, Dk. Slaa alisema: “Ni kweli tulikuwa tumealikwa kwenye mdahalo pale ITV (leo) jana saa 3, nilipofika nilikutana na Nape, nikamsalimu nikajua kuwa alikuwa amemsindikiza Kinana, lakini nilipomuuliza mwendesha kipindi kwamba Kinana yuko wapi, alisema amepata udhuru hivyo hajafika.

“Nilimwambia Nape wewe si saizi yangu, sitaweza kuongea katika kipindi hiki kama Kinana hayupo, hivyo kipindi hiki kiahirishwe hadi Kinana atakapokuwa na nafasi ya kuja,” alisema Dk. Slaa.

“Haiwezekani mwenzangu akaahirisha ghafla kuja kwenye kipindui halafu nisipewe taarifa na badala yake nikatumiwa Nape, Nape si saizi yangu,” alisisitiza Dk. Slaa.

Taarifa zaidi zinasema kuwa baada ya kuahirishwa kipindi hicho, Nape na Dk. Slaa walisalimiana na kuagana. “Naamini siasa si uadui, niliongea na Nape nikamuuliza Kinana yuko wapi, alisema alikuwa amepata udhuru, akanipigia simu nije,” alisema.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu suala hilo, Nape alisema alikwenda ITV badala ya Kinana, kuangalia maudhui ya kipindi hicho ili aweze kushauriana na Kinana na kuamua kuja au la.

“Mimi ndiyo msemaji wa chama, katibu mkuu hawezi kualikwa mimi nisiwe na taarifa, mimi ndiyo napaswa kwenda na nilikwenda nilipokutana na Dk. Slaa tukaelezwa, Dk. Slaa alishauri kuwa inafaa kualika watu wenye hadhi zinazofanana, yaani makatibu, hivyo mimi niliondoka nikamwacha Dk. Slaa, nadhani alirekodiwa kwa kuwa walisema wanaweza kurekodi mtu mmoja mmoja na katibu mkuu wetu anaweza kwenda siku nyingine kurekodi,” alisema Nape.

Kinana mwenyewe alipotafutwa kwa simu yake ya mkononi kuzungumzia suala hilo, hakuweza kupatikana kwani simu yake iliita bila kupokewa.

via: Tanzania Daima Mei 16, 2013
                   Nape Nnauye / Alhamisi, Mei 16, 2013

Toka jana nimekuwa nikisoma kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu hoja ya " NAPE, KINANA NA DR. SLAA" juu ya kipindi kilichodaiwa kuandaliwa na ITV. Leo kwa uzito mkubwa stori hiyo imebebwa na gazeti la Chadema la TanzaniaDaima. Kwa gazeti hili ni stori inayouza gazeti lao leo.

Niseme toka jana niliposoma propaganda ya Tandaleone nilishangaa lakini nikajipa muda kujua msingi wa propaganda ile. Baada ya muda nikaona majibu ya Babu Dr. Slaa nikayashangaa pia japo si sana, bado niajipa muda. Jioni nikapigiwa simu na mwandishi wa TanzaniaDaima kuulizwa juu ya hiyo stori, nikasema wameanza sasa kuja hadharani na makusudi yao naanza kuyafahamu. Pamoja na kujitahidi kueleza kilichotokea bado matokeo ni Lead Stori ya TanzaniaDaima leo inayodai eti Kinana kamkimbia kiaina Babu Dr.Slaa!!!! Raafiki yangu mmoja asub alipoona gazeti la Chadema limeandika vile akanitania akasema nilitegemea UHURU waandike "KINANA AMPUUZA BABU DR. SLAA" nikamwambia UHURU linafanya kazi ya nchi si ya Chama pekeake ndo maana limekuwepo hata kabla ya CCM kuwepo!!

Lakini ninachotaka kusema hapa ni propaganda kama za Gazeti la Chadema leo ni dalili za kufilisika sana kisiasa kiasi kwamba hhata jambo dogo sana linageuzwa kuwa jambo kubwa na linalodhaniwa linaweza kutumika kipropaganda. WASWAHILI WALISEMA kwa sisimizi hata kifuu cha nazi kwake ni sawa na bahari!Pengine tungemsaidia sana mwajiri kwa kumfanyia utafiti kwanini ofisi za wilayani na mikoani za taasisi anayoiongoza zinafungwa kwa kasi ya ajabu.

Sourc

0 comments: