Mkutano kati ya rais Yanukovych na viongozi wa upinzani Ukraine
Rais wa Ukraine, Viktor
Yanukovych, na viongozi watatu wa upinzani nchini humo wameafikiana
kufanyia mabadiliko sheria iliyozua utata ambayo ilipiga marufuku
maandamano. Pingamizi dhidi ya sheria hiyo imezua rabsha kati ya
waandamanaji na polisi wa kupambana na ghasia, na kusababisha vifo vya
zaidi ya watu watatu.
Kadhalika bwana Yanukovych amerejelea ombi lake
la kumtaka kiongozi wa upinzani, Arseniy Yatseniuk, kukubali uteuzi wake
katika wadhfa wa waziri mkuu, wadhfa ambao bwana Yatseniuk alikataa.Tangazo kuwa sheria iliyopiga marufuku maandamano itafutiliwa mbali lilitolewa kwenye mtandao rasmi wa rais Victor Yanukovich. Bunge linatarajiwa kupigia kura hatua hiyo ya kubadilisha sheria baadaye hivi leo.
Chama cha bwana Yanukovich cha Party of Regions kinajivunia idadi kubwa ya wabunge lakini bado haijabainika iwapo wabunge hao watakubali kupiga kura kufutilia mbali sheria hiyo.
Bwana Yanukovych na viongozi hao watatu wa upinzani kadhalika wamekubaliana kutolewa msamaha kwa waandamanaji waliokamatwa. Lakini hili litatekelezwa tu ikiwa wanaharakati wataondoa vizuizi walivyoweka katikati mwa mji mkuu wa Kiev na kuondoka katika majengo ya serikali. Olena Lukash ni waziri wa sheria.
Maandamano yamekuwa yakienea katika maeneo mbali mbali nchini Ukraine
Na baada ya mazungumzo hayo mmoja wa viongozi wakuu wa upinzani aliyekuwa mwanamasumbwi Vitali Klitschko kutoka chama cha Udar alizungumza na wanahabari.
"Mazungumzo ni marefu na pia magumu. Napenda kutaja maswala kadhaa ambaye yanajadiliwa na nadhani hapo kesho tutapata fursa ya kuyatathmini kwa ndani. Watawaachilia watu waliokamatwa na kuwapa msamaha. Pia sheria yenye aibu inayopiga marufuku maandamano tangu tarehe 16 mwezi januari kinyume na katiba itafutiliwa mbali," alisema Vilai Klitschko.
Mazungumzo kati ya pande zote mbili yalianza wakati maandamano ya kuipinga serikali ya Ukraine yalipogeuka na kuwa vurugu na kisha kuenea katika maeneo mengine ya nchi juma moja lilopita. Wanaharakati wameedelea kuteka medani ya mji mkuu wa Kiev pamoja na majengo ya serikali katika miji kadhaa nchini Ukraine, wakikata kuondoka hadi pale bwana yanukovich atakapojiuzulu.
0 comments:
Post a Comment